Kwanini unibadilishie mfumo wangu wa maisha??!!


ni kweli tasia, maamuzi yako huwezi kuyamiliki 100% kuna vitu ambavyo lazima mjadili mfikie muafaka. Ina maana huwezi kujiamulia.
Ila suala la interests za mtu sio suala la mtu mwingine kulifanyia maamuzi.
Unaweza kujifunza kukikubali kile anachopenda mwenzio. Au waonaje?
 

mpendwa maneno gani yana ukali nikayaedit? Wala sina ghadhabu. Lisred lenyewe tu limekaa kighadhabu ghadhabu.
B2T: huyo binti ameshamwambia rafiki yangu kuwa hawezi kubadilika. Rafiki yangu ndio hajui kama aendelee nae tu hivyo hvyo au achape lapa.
 

well said. Mpasome hapo juu.
 

Nakubaliana na we 100%, mi sidhan kama MAMBO ya club,vimini,pombe kwa mwanamke ni jambo la kawaida kwa jamii ye2 hasa ya kitanzania, hebu angalien skendo za wasanii wa kike kama irene uwoya, ambavy alikuw nazo,ameolew halaf mambo ambayo alikuw anafany akayaendeleza! Hii haileti picha kabisa ktk mahusiano, HUYO mwanaume alikuvumilia hapo mwanzo na anapotaka ubadilike anakuepusha na mengi ambayo we hutayaona! Kwahyo msikiliz na ubadilike! Lakini yote tisa, kumi ni kwamb inawezekan Mwanamke anapesa, na elimu ambayo inampa kibur cha kutotaka kubadilika anaona hata kama huyu mwanaume atamwacha atapata tu mwingine! Kwahyo hana shida sitarehe kama kawa.. Usemi ni ule ule ''PATA PESA TUJUE TABIA YAKO''.. Na ki2 kingine kama hutak kuacha hiyo tabia ambao mi siipend kabisa, unaonaje utakapo pata watoto, na 2najua tabia ya mtoto inatoka kwa mzazi hasa Mama. Je huoni utawafundisha watoto wako tabia mbaya ambayo itapelekea kuwa na wenz wengi, mimba, na tabia chafu ambazo haziitajiki katika jamii.. Kuwa na akili ya kuangalia mbele si ulipo sa hvi.
 
BAK & WISELADY.
Mmeongea kitu kuombana au kuelekezana kwa utaratibu. Kweli ni vizuri hata kama unataka kumbadilisha mtu ufanye kumuomba.
Habari za kumwambia usipoacha kufanya hivyo mimi na wewe basi inakuwa kama unamlazimisha kinguvu.
Wakuu AFRODENZI, KING'AST, NEWDAWN na JUMALESO nimewasoma. Mmeongea vyema sijaona pa kuwachallenge.
 

kwa vi2 vizur mi sipingi kabisa, kama ni kuongea na wa2,kwenda beach halaf jamaa anakukataza hapo atakuw anakosea, lakin si kwa mambo mabaya na ya aibu HUSNINYO.. Kwa mfano mi napenda kuangalia Movies, mpira wa basket, lakin ikitokea mpenz wangu akasema niache, inabidi nimuulize kwanin anataka niache ,na kuna madhara gan kwenye hvyo vi2.. Na kama atatak niache 2 kisa amependa kwel cdhan kama kunaleta mantik.
 

Kwa mfano ulitongozwa na huyo mwanaume club tena usiku wa manane, mkakubaliana, mkapendana na mkaanza kuwa wapenzi. Lakini kila weekend huyu mpenzio anapenda kwenda club (peke yake) hadi majogoo. Tabia hiyo haikupendezi, unapomuuliza anasema ulinikuta napenda kwenda club kwa hiyo naomba uniache nifanye ninachopenda. hapa sasa itakuwaje, utamwacha aendelee kufanya anachokipenda hadi yeye mwenyewe aamue kuacha?
 

The sentence I hate most in a marrital relationship.

Huwa najiuliza, kwani wewe mwanaume ndio unaamua ndoa iendelee au isiendelee, kwa kuwa tu mapendekezo yako hayajatimizwa? Tena wakati mwingine unakuta vitu vingine ni so trivial.

Je nami nikaanza kuitumia hiyo sentensi kwenye mambo ambayo siyapendi, hiyo nyumba inasonga kweli?

Nadhani hao wanaume wanaopenda kutumia hiyo sentensi wajiulize, je mimi mpenzi wangu anapenda kila kitu kutoka kwangu? Hebu tukae tuongee tuone nini tunaweza fanya kuyamanage mapungufu yetu bila kutishiana kuachana.
 

kwa kesi hii kama anapenda kwenda club mwambie muende wote ila sio umkataze kabisa. Unaweza ukamkataza akaacha huku moyo wake unasononeka matokeo yake siku haupo anatoroka. Kwanini umjengee mazingira ya kujiiba iba? Au unakuta mtu anakuwa kwenye uhusiano ila hafurahii kutokana na kushindwa kufanya vitu ulivyomkataza.
Kwanin umnyime mtu uhuru wa nafsi?
 
The sentence I hate most in a marrital relationship.
Hebu tukae tuongee tuone nini tunaweza fanya kuyamanage mapungufu yetu bila kutishiana kuachana.

umeongea vyema. Kuna watu wanajua kutoa vitisho kwa wapenzi wao.
Sasa mtu mzima mwenzio unamtisha tisha kama mtoto sijui ili iweje.!
 
WATU WAZIMA HAWATISHIANI BALI WANAELEWESHANA JUU YA JAMBO LOLOTE LINALOONEKANA SI ZURI KWAO.
MPENZI/MKE/MUMEO KUKUSHAURI JAMBO UNALOFANYA KAMA ANAONA SIYO ZURI SI VIBAYA,
NA HAPO UNA HIARI YA KUKATAA AU KUKUBALI MOJAMOJA, AU KWA KUPEWA MUDA MFUPI WA KUJIREKEBISHA.
KUSIKILIZANA NA KUELEWESHANA NI SEHEMU YA MAPENZI.

HAUPASWI KUMWAMBIA MWENZI WAKO KWA SAUTI KALI NA USO MKAVU kwa mfano ETI USIPOACHA POMBE NAKUACHA.....
HATA KAMA HAUPENDI KIWANGO CHA POMBE ANACHOKUNYWA BASI KUNA JINSI YA KUMWAMBIA NA KUMPA MUDA
PIA WA KUBADILIKA,USITEGEMEE LEO LEO UMEMWOMBA JAMBO FULANI AACHE BASI LEOLEO AACHE KWELI mmh! huyo mtoto au mtuzima??

Binadamu tunaweza kubadilika kutoka wema kwa ubaya au ubaya kwa wema.
Lililo muhimu ni kuelimishana na subira, pamoja na matumizi sahihi ya njia ya kumbadilisha mtu.
 

Anakwambia hapendi mwende wote, yeye ana enjoy kwenda club peke yake. Ukizingatia kuwa hata siku mlipokutana alikuwa peke yake..
 
NN ngumu sana banaa hiyo mtu mzima kubadilishwa tabia labda aamue mwenyewe tu

Ewaaaa.....hapo bolded ndo umegonga Ikuli mazee. Na ninaamini mtu afanyaye mabadiliko mwenyewe hayo mabadiliko yatakuwa ya dhati. Lakini hii ya kusema sijui nimbadilishe fulani tabia yake....sijawahi mimi kuiona. Huenda wapo wanaobadilishwa tabia na wenzao lakini mimi sijawahi kuwaona.

Halafu mara nyingi wanawake ndo huwaga na mawazo ya kuwa wanaweza kuwabadili wenza wao.
 
Kweli kabisa nilishawahi kushuhudia mwanamke anamkataza mwanaume wake asiwe anafanya mambo aliyokuwa anafanya zamani ambayo kimsingi sio kwamba yangebadili mfumo wa maisha waliyonayo matokeo yake jamaa akawa worse zaidi kuliko ambavyo alivyokuwa mwanzoni
 
Halafu mara nyingi wanawake ndo huwaga na mawazo ya kuwa wanaweza kuwabadili wenza wao.[/QUOTE]


Hata wanaume pia huwa na mawazo hayo. mf anatongoza mwanamke ambae hajatulia kabisa lakini anajiambia mie huyu mwanamke nikifanikiwa kumpata, ntamtuliza tu.. sasa sijui kama huwa wanafanikiwa kuwatuliza!
 
Anakwambia hapendi mwende wote, yeye ana enjoy kwenda club peke yake. Ukizingatia kuwa hata siku mlipokutana alikuwa peke yake..

unamuacha aende mwenyewe.
Mpe uhuru.
 
Muanzisha thread hana hekima la sivyo iko chini ya kiwango cha kawaida.

Pole zako bibie asiyefunzwa na ***** atafunzwa na dunia. You will learn through you mistakes.

Mungu akutie nguvu, uone mbali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…