Kwanini unibadilishie mfumo wangu wa maisha??!!

Ukipenda kisawa sawa unabadilika. Tatizo watu wako kwenye relationship kimtego mtego. Mimi kuna watu nawajua wamehacha sigara (which is very difficult) kwa kuwa wake zao hawapendi including OBAMA. Ila tabia nyingine ni addiction kwa hiyo kuacha ni ngumu. Zile ambazo ni rahisi kuhacha mimi nashauri mtu ahache tu ndo kupenda. Na ukiona inakuwa ngumu kuhacha hujue hujapenda bado tafuta pengine. Nina rafiki yangu alikuwa mlevi hamna mfano yaani anamaliza nusu kreti bila kulewa na ni msichana. Ukimuuliza anakwambia baba yao aliwazoesha kunywa toka wadogo. Wakati tuko college alikuwa mwepesi kukubali kwenda out na boys sababu wamnunulie bia za bure. Sasa hivi kaolewa na jamaa ambae si mywaji, nae amehacha kabisa. Where there is love nothing is impossile.
 
Labda kama amefanya research kwa nini huyo dada hajatulia. Ila mimi namjua mama mmoja aliolewa na pilot yeye alikuwa anauza baa na alizaa mtoto kwenye hiyo kazi yake. Jamaa kaoa. Huwezi amini yule mama ukiambiwa alikuwa muuza bar. Anajiheshimu kuliko maelezo na ni mfanyabihashara mzuri. Mumewe sasa ndo kicheche.


Halafu mara nyingi wanawake ndo huwaga na mawazo ya kuwa wanaweza kuwabadili wenza wao.


Hata wanaume pia huwa na mawazo hayo. mf anatongoza mwanamke ambae hajatulia kabisa lakini anajiambia mie huyu mwanamke nikifanikiwa kumpata, ntamtuliza tu.. sasa sijui kama huwa wanafanikiwa kuwatuliza![/QUOTE]
 
Muanzisha thread hana hekima la sivyo iko chini ya kiwango cha kawaida.

Pole zako bibie asiyefunzwa na ***** atafunzwa na dunia. You will learn through you mistakes.

Mungu akutie nguvu, uone mbali!

amina caroline danzi!
 
Ndio maana watu husema mke hapatikani club!
Kuna maeneo ya kupata mke kama vyuoni au kanisani. Ndio maana mtu kama umemaliza shule bila serious relationship you are likely to remain single or end up in wrong relationship. Ushawahi sikia mtu mzima na shahada zake anakwambia dada/kaka nitafutie mke? Alijisahau akakazana kusoma bila kuangalia wachumba pia!

 

umeongea vyema nyumba kubwa.
Inawezekana bidada hajampenda na ndio maana amekuwa mgumu kuacha anayokatazwa.
 

na wale ambao wameoa na hawajafanikiwa kufikia elimu ya vyuoni? kwani wote walioanza mahusiano vyuoni wameishia kwenye ndoa?
mke anapatikana kokote, inategemea unaangalia vitu gani..
 
hujawahi kuona?
Inabadilishwa ingawa ni ngumu.

Ni nadra sana kuona. Wote niwajuao mimi waliojidai wamebadilika ama waliirudia hali yao ya zamani baada ya muda mfupi tu au hawakubadilika na walipotenda walijificha wasionekane. Ndiyo maana mabadiliko ya kweli na ya dhati yanatoka kwa mtu mwenyewe na si kwa shinikizo la nje!!
 
Mtizamo wako bado ni ghasi Husniyo na nafasi ya kusuluhisha bado unayo kama unaona muhali basi tafuta mtu aseme naye huyo Binti. Hoja ya jamaa ya kumtaka binti aache pombe ni ya msingi kwa kuwa jamaa anatizama mustakbali kumbuka wapendanao hujitahidi kufanya yale yasiyomkasirisha mwenza. Usimlaumu ya jamaa kwa kuwa alimpenda Binti ilihali akijua kuwa ni mkata maji sasa unataka kufunga mlango ili wakata maji wapendwe na wakata maji tu? Huwatendei haki ondosha muhali na jikubalishe kuwa pombe si rafiki wa mahusiano bali ni adui wala haijengi heshima bali inabomoa
 
Nilichomaanisha you need time to study your partner if you need a lasting relationship. Hata ambao hawajasoma ni wachahe wanatafuta mume/mke club!

na wale ambao wameoa na hawajafanikiwa kufikia elimu ya vyuoni? kwani wote walioanza mahusiano vyuoni wameishia kwenye ndoa?
mke anapatikana kokote, inategemea unaangalia vitu gani..
 

mimi sisupport pombe na wala sio mnywaji kabisa ila naheshimu interests za watu.
Naheshimu kile nini watu wanapenda as long as hakiniaffect kwa namna moja au nyingine.
Jamaa nimemwambia yeye ndiye mwamuzi wa mwisho. Anyoe au asuke.
 
Kuna mtu namfahamu alioa mwanamke na mimba ya miezi mitatu kisa dada zake wamemtafutia yeye alikuwa busy na kitabu kuja kushtuka age mates zake washaolewa. Madada wakamtafutia shosti yao mume (kaka) kumbe binti ana mimba ya miezi mitatu. Jamaa ikabidi atoe talaka na mpaka leo hajaoa anaona nuksi maana ilikuwa bonge la harusi.
 

...kubadilika kufuatana na umri, majukumu ya kifamilia na maisha muhimu. Ndio maturity hiyo.
 
Ni sahihi kumbadilishia mtu utaratibu wake wa maisha tena kinguvu namna hiyo?
Nawasilisha.
Ndio ni sahihi kubadilisha staili ya maisha manake ukumbuke ukiingia kwenye uhusiano umejifungia baadhi ya mambo iwe mkaka au mdada
Michalle alimwaidi Obama kumpa support kubwa during kampeni ila iende sambamba kwa yeye Obama kuacha uvutaji wa sigara
 

unampenda mtu yes
lakin chapombe na anataka mzae ....lakin anatumia pesa zote kwa pombe na anarud saaa8 usiku daily..anakuwa mchafu


je apo ukiombwa ubadirike nayo inakuwa umeingiliwa?/autapenda?
mi navyojjua mpz akikwambia john badirika acha A acha b,c,d basi ni mara nying ni kwa manufaaa kwenu
awez kukukataza usiende kazn,usisome....apana
so unapobadirishwa usikaze shngo cz smtimes unakosea sema hujijui km unakosea ...ikkitokea mtu akakkusahihisha basi huna bud kujichek marambili na kufanya correction...kinyume na apo ni UJEURI WA KIJINGA.
 
He unibadilishe ili iweje?? Ulivyonipenda hukuona??? Mambo mengine ya kupimiana hewa mie siyataki........

Huwezi kula kubwa tusipangie laga nakunywa na uliunikuta hivyo iweje unipangie kwa sasa????
 
unampenda mtu yes
lakin chapombe na anataka mzae ....lakin anatumia pesa zote kwa pombe na anarud saaa8 usiku daily..anakuwa mchafu

Duh! Yaani kabisa utakuwa umekosa mwingine anayekufaa hadi uhangaike na kumbadilisha chapombe mchafu? Haya bana to each his/her own. Wewe kama kazi ya kumbadilisha huyo chapombe wako mchafu unaiweza powa tu. Si maisha ni yako bana....
 
He unibadilishe ili iweje?? Ulivyonipenda hukuona??? Mambo mengine ya kupimiana hewa mie siyataki........

Huwezi kula kubwa tusipangie laga nakunywa na uliunikuta hivyo iweje unipangie kwa sasa????

si ndio hapo!!
 
unampenda mtu yes
lakin chapombe na anataka mzae ....lakin anatumia pesa zote kwa pombe na anarud saaa8 usiku daily..anakuwa mchafu

mmh! Huyo chapombe mchafu sijui utakuwa ulimpendea nini hali ya kuwa ulishajua hivyo alivyo.
Kwa kesi hii napendekeza umwelezee vile usivyovipenda kabla hamjaingia kwenye mahusiano ili ujue kama yupo tayari kubadilika au lah! S mshamaliza mwaka mzima ndio unaanza ooh! Mimi pombe zako sizipendi, ooh acha hiki, haipendezi.
 
ndege wawili huruka pamoja!!!

tangu mwanzo, siku ya kwanza kabisa wangekalishana chini na kuelezana wakipendacho na wasichokipenda, kila mtu aridhie tabia ya mwenzie, na kama kuna tofauti mmoja akubali kubadilika.

lkn ss inakua ngumu kama hawakuelezana tangu mapema, kuja kubadili tabia ya mtu ni ngumu sana otherwise Mungu aingilie kati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…