Kwanini ushairi haupewi thamani ndani ya nchi hii ?

Kwanini ushairi haupewi thamani ndani ya nchi hii ?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Nimejaribu sana kutafakari lakini nakosa majibu ni kwanini Tanzania na si Kenya ama kwingine ?
kiswahili kwa asilimia mia moja kinazungumzwa sana nchini Tanzania tena kwa ufasaha na urahisi ambao wengi wana uwezo wa kukielewa.
ndani ya kiswahili kuna fani ya ushairi ambayo inachangia sana kuenea kwa kiswahili lakini cha ajabu "KWANINI USHAIRI HAUPEWI THAMANI NDANI YA NCHI HII ?
Unapofuatilia vyombo vya habari vya Kenya,television na magazeti hautokosa makala ya kiswahili na ushairi.
unaposoma gazeti la "TAIFA LEO nchini Kenya utakuta na na makala na tungo kibao za washairi lakini kwanini siyo Tanzania ?
mbali la "MCL/GAZETI LA MWANANCHI,kwanini magazeti mengine hayatoi kipambaupele kwa washairi wa nchi ?
washairi ambao kila siku hushinda na kukesha wakiilinda lugha ya kiswahili ni kwanini hawapewi thamani katika nchi yao,kwani kazi zao hazilindwi ?
najiuliza tena,au hatukipendi kiswahili ?
 
Ibin Batuta
alizulu pwani ya Afrika Mashariki...
 
Pole sana ndugu yangu, kipaumbele cha kwanza inatakiwa sisi wenyewe wanançhi, je wananchi wa sasa wana utayari wa kutunga na kusoma hayo mashairi? Zamani nilikuwa napenda sana akina Andanenga, shabani mkadalu nk, mashairi yao yalikuwa yanafundisha kuburudisha, Kwa mfano Mzee Mkadalu siku anastaafu pale RTD alienda na mashiri mawili lile moja lenye kichwa " kilio hichi ntaliaje mwenzenu" linavuta sana hisia. Zamani kipindi cha mashairi hatukosi, ila siku hizi Mange, Shilawdu, Diamond na Zari na siasa ndio vipaumbele vya vijana, bila kusahau kubet. Kwa hiyo naona shida si magazeti tatizo ni wasomaji, leo toa gazeti njoo na mbinu 10 za kubet ili ushinde, utauza mpaka basi
 
Basi tukubali kuwa vipaumbele vya taifa hili ni shilawadu,kubeti,diamond.
lakini kama kipaumbele siyo kiswahili,ni kwanini kiswahili kiwe lugha ya taifa.
 
Back
Top Bottom