Author
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 1,715
- 8,058
Wana JF habari za leo, nimeona nizungumze hili swala kwa wote wanaonzisha nyuzi humu JF. Unapoanzisha uzi unategemea member wengine wafurahi, wajifunze na zaidi wachangie kwenye uzi wako. Shida ni kwa sisi waanzisha nyuzi kutokuonyesha kuwa tumefurahi kwa wao kutumia muda wao kuchangia kwenye nyuzi zetu. Ushauri wa Bure: member akichangia kwenye uzi wako fanya ku-like mchango wake; kwa kutumia muda wake na kuona haja ya kuchangia kwenye uzi wako. Mfano mzuri mimi mtu akichangia kwenye uzi wangu nampa 'Like' kila anapochangia...Na hilo limefanya nipate like nyingi kwenye nyuzi zangu...Nawasilisha
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app