Kwanini usipokuwa na hela njaa inauma tu wakati wote?

mr pipa

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
3,074
Reaction score
6,472
Ile unatembea kitaa kila baada ya lisaa njaa hiyoo, hapa sio kwamba hujala gheto ila tu pesa mfukoni hakuna.

Ia siku ukiwa na pesa unaweza dumu siku nzima hata hamu ya kula unakosa, unakula ile ya kujilazimisha zaidi utatamani soda au maji.

Wakuu ni mimi pekee yangu au?
 
Ndio kwanza nasikia kwako, huenda ni wewe tu uliyerogwa
 
Taarifa inakuwa imeshapelekwa kwenye ubongo kuwa mfukoni patupu hivyo ubongo wenyewe unaanza kuwa mtupu kama mifuko ilivyo hivyo ubongo unakuwa na njaa kabla ya tumbo.

Sasa ukizichanganya hizo njaa mbili za ubongo na tumbo njaa yake inakuwa kama ya Maharage Chande mkuu. Ahsante.
 
Alafu unakuwa unatamani vyakula vya kitoto kitoto unajikuta unahamu ya kula kashata
Ila siku ukiwa na hela mtu akikuambia naomba uninunulie kashata,unamjibu acha zako wewe ukila kashata watoto watakula nini?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahahahaha
Ni vile mwili unajua kabisa hakuna mafuta mfukoni lazimamukate tamaa na nyongo inakuwa network search kwa ssna🤣
 
Hofu na wasiwasi ni mbaya sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…