Magari yote yenye kuweza kwenda spidi kubwa yana usukani pembeni (au kulia au kushoto). Lengo lake ni kurahisisha dereva kulitawala gari. Na hii ina msaada zaidi pale anapopishana na gari nyingine ili kuhakikisha anapima umbali wa gari lake na wa lile linalokuja mbele yake ili yasigongane au kukwaruzana. Ndiyo maana inashauriwa kama utaratibu wa nchi ni kuendesha magari LHD au RHD basi magari yote yawe na usukani unaoendana na utaratibu wa nchi husika.
Ni magari yanayoenda polepole kv trekta, buldoza, nk yanakuwa na usukani katikati kwani hayana hatari ya kukutana na mazingira mengi hatarishi, mfano kukutana na magari mengi barabarani tena kwa mwendo kasi sawia.