Kwanini UTOSI wa mtoto unacheza?

Hakika Nguto.
http://s07.jamiiforums.com/mini/uyE8/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/
 
Zinatwa fontanelle.. Ni sehemu ya maungio ya mafuvu ya kichwa..kuchezacheza inonesha kuwa hapajafunga vizuri..na huwa panakaa sawa baada ya muda..
 
Ok,ninachifikiri kila sehemu ya binadamu ipo jinsi ilivyo kwa sababu ya kufanya kazi fulani,sasa kwa mtoto kwanini kunakuwa wazi na panafunga baada ya mda fulani,angezaliwa kukiwa kumefungwa ingezuia nini
Wewe kwani hujona kitovu cha mtoto kinaning'inia mpaka ukifika wakati kinaanguka
halafu ndo anakuwa kama wengine, si hapo tu panapokuwa wazi hata mdomoni mtoto
anazaliwa bila meno akikua ndo yanaota.
 
Ok,ninachifikiri kila sehemu ya binadamu ipo jinsi ilivyo kwa sababu ya kufanya kazi fulani,sasa kwa mtoto kwanini kunakuwa wazi na panafunga baada ya mda fulani,angezaliwa kukiwa kumefungwa ingezuia nini
Hiyo ni kazi ya aliyetuumba na hapangiwi kwa vyovyote vile.
 
Fuvu la kichwa lina pande mbili,ukizaliwa pale kati bado mfupa wa fuvu unakua haujafunika hivo mapigo ya moyo yanapoleta damu kichwani ndo ubongo vile unadunda pale kati,anavokua mifupa inaungana hadi kufunga kabisa na kuwa migumu
 
Usijali,mtoto uzaliwa na mibonyeo mingi katika kichwa,ambayo kitaalamu wanaiita softspot au fontanelles

mbonyeo uliomkubwa na unaodumu kwa muda mrefu ni wa juu ya kichwa(utosini) unaoitwa anterior fontanelle,mbonyeo huu utoweka baada ya mwaka mmoja mpaka mmoja na nusu baada ya mtoto kuzaliwa.

mibonyeo hii husababishwa na ulaini wa mifupa inayounda fuvu wakati mtoto anapozaliwa kutokana na kutokuwa na madini ya kutosha kuifanya mifupa ya fuu la kichwa kuwa imara na gumu.

kazi kubwa ya mibonyeo hii ni;

-kuifanya mifupa ya kichwa kuwa flexible na kuiwezesha kutembea tembea huku na huko kukiwezesha kichwa cha mtoto kupita kunako uke wa mama wakati wa kujifungua.

-mbonyeo wa juu ya utosi unaupa nafasi ubongo wa mtoto kukua.
 
-mbonyeo wa juu ya utosi unaupa nafasi ubongo wa mtoto kukua.
Nimekupata.Huo mbonyeowa juu,ni kws namna gani unaupa ubongo nafasi ya kukua na je pakiziba ubongo unafikia mwisho wa kukua?
 
The hammer,mbonyeo unaouona kwenye utosi si kwamba upo peke yake inakuwa sehemu mbali mbali kwenye kichwa tofauti ni kwamba mingine ni midogo mno.

mibonyeo hii hua na nafasi kwa ndani inayowezesha ubongo kukua.

ubongo utaendelea kukua mpaka fuu la kichwa(skull) litakapokuwa gumu na hii ni kati ya miaka mi 3 mpaka mi 5,baada ya hapa ubongo usimama kukua na uendelea kudevelop tu.
 
Ok,ninachifikiri kila sehemu ya binadamu ipo jinsi ilivyo kwa sababu ya kufanya kazi fulani,sasa kwa mtoto kwanini kunakuwa wazi na panafunga baada ya mda fulani,angezaliwa kukiwa kumefungwa ingezuia nini
tho my son nimemzaa kafunga hajawah dunda utosi. sio lazma kila mtoto adunde utosi pia
 
Na kuna wale wanaoamini uchawi nasikia hutumia sana fuvu la mtoto mchanga kwenye mambo yao,
ni wale watoto wanaozaliwa lkn kwa bahati mbaya wakafariki kwa muda mfupi au wanaozaliwa njiti na kushindwa kuishi,
Ebu nyie wachawi tuambieni kwa nini munapenda mafuvu ya watoto wchanga?
 
tho my son nimemzaa kafunga hajawah dunda utosi. sio lazma kila mtoto adunde utosi pia
Ila nafikiri mwenyewe uliuliza kwa daktari akakuhakikishia hilo kwasababu sikawaida hilo kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…