Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Matukio yote ambayo Vijana wanatekwa hasa Wenye mlengo wa kukosoa serikali, UVCCM haijawahi kutoa tamko la kukemea hata kinafiki tu. Tukio la karibuni zaidi ni la kijana Edgar Mwakabela @SATIVA ambaye alitekwa Dar na kutupwa Katavi baada ya kupigwa risasi ya kichwa lakini Mungu mkubwa ikamvunja taya tu.
Alipohojiwa akataja baada ya kutekwa alilazwa karakana ya kituo cha Polisi Oesterbay kisha Arusha na baadaye Katavi ili akauawe. Kwa siku zote kelele zikipigwa mitandaoni huku Polisi wakituhumiwa UVCCM walikuwa kimya utadhani wao ndio Polisi wanaotuhumiwa.
Kinachonishangaza zaidi ni pale Zitto Kabwe aliposema ameongea na Rais Samia na ameahidi kulipia sehemu ya gharama za matibabu na akafanya hivyo, ghafla UVCCM wameibuka na kumpongeza Rais.
Hii ni Aina mbovu ya uhuni na kukosa busara. Unakaa husemi chochote nilipotekwa, Niko hospitali mahutuki uko kimya, ghafla unasikia kiongozi Fulani katoa hela ya matibabu unakurupuka kupongeza.
Ndo màana Kwa ukimya wao hata Mwenyekiti wao alipotoa mchango alirudishiwa mchango wake. Hii ilikuwa sahihi hata vijijini inafanyika. Mtu kapotea kijijini Vijana tunatoka kwenda kumtafuta wewe unakwenda kufungua Duka lako, kesho maiti yake ikipatikana unakuwa wa Kwanza kuleta ramborambi kwenye daftari la Mtaa Kwa nini tusikurudishie?