SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Moja ya changamoto kubwa ya Uwanja wa Mkapa ni kuharibika mara kwa mara kwa sehemu ya kuchezea kutokana na jua kali au mvua.
Leo nakuja na pendekezo kuntu, kwa nini tusiezeke bati kumaliza changamoto hizi? Kule Singapore wana uwanja ambao paa lake linaweza kufungwa au kufunguka kulingana na mazingira ila ujenzi au maboresho ya namna hii ni gharama sana.
Tukumbuke pia viwanja vingi duniani vikijengwa huwa wanaweka alama fulani katika muonekano ya utambulisho wa jamii ya watu wale. Nakumbuka kule Qatar kuna uwanja uliojengwa kwa mfumo wa kofia ya kiarabu. Sina uhakika ile design inayozunguka uwanja wa Mkapa inaashiria nini katika tamaduni zetu ila bati utalikuta kila mtaa na kitongoji cha nchi hii.
Bati ni moja ya nembo ya ujenzi wa kitanzania, tulienzi kwa kuliezeka uwanja wa Mkapa. Tutakuwa tumeua ndege wawili kwa jiwe moya.