Kwanini video za ngiri zimekuwa maarufu sana mtandaoni?

Joined
Oct 6, 2024
Posts
147
Reaction score
303
Mimi Bibi Yenu, licha ya kuwa pensioner lakini najihangaisha kwa KAZI za mikono na talanta alizonipa Maanani.

Bidhaa zangu nauzia mtanfaoni, hivyo huwa nabahatika kukutana na vimbwanga vya huko.

Ila nimegundua ngiri kwa sasa amekuwa maarufu sana, katika video kumi huenda tatu ni za ngiri, nini kimetokea?

Wazee tusaidiwe taarifa
 
Nimesoma heading tu nikawahi kucomment kabla kisimu changu cha mchina hakijazima charge na umeme tanesco wamekata.!
Back to the topic.. Sababu kubwa ya ngiri kutrend sana mitandaoni ni kwamba ngiri ndio ugonjwa pekee unaowasumbua wanaume wengi hasa kipindi cha baridi
Yaani mnyama huyu akikuingia haijalishi wewe ni mbabe kiasi gani utanyooka na kulala sakafuni ukiwa umelegea huna nguvu hata ya kushika simu uingie JF!
 
Nabii hana heshima kwao huko duniani anatrend balaa ila hapa kwetu wapo wengi sana ila hatuna habari now ..
Tanapa kitenge chenu cha marketing kimelala sana kwa sasa ukiwapa promo hao wadudu watalii wanakuja kama wote mtazubaa kenya watachukua hiyo fursa then mlalamike badae..
 
Anakuingiaje?
 
Mi nilijua ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume...🤪.

Akili yangu imejiuliza.....
Hivi mwanamke akinywa dawa ya kuongeza nguvu za kiume nini kitatokea.....🤔🤔🤔

Kifaa gani kwenye mwili wa mwanamke kitasimama imara kwa masaa mawili baada ya kunywa viagra/dawa ya kuongeza nguvu za kiume?
 
Na mie mzee mwenzako nilikuwa nawaza vivyo hivyo,
By the way vipi ubaridi wako na hali yako nyingine kwa ujumla wako kama ulivyo. 🙂
 
Wanasema jopo la kupima speed za wanyama walipokuwa field siku hiyo ngiri alikuwa amejipumzisha shimoni kwake kwahiyo sifa za mnyama mwenye mbio, mfalme wa pori zikampitia pembeni😆😆

Hii ni wiki ya Mr. Warthog A.k.a Ngiri au Pumba, enjoy bibi angu😃
 
Mshenzi yule ana maamuzi magumu, anaezafukuza hadi honey begger,
 
Yes, ni Pumba kwenye The Lion King, mwenzake alikuwa anaitwa Timo. Huu mkanda wa video nilimnunulia mjukuu wangu wa kwanza Bar Jonnah mwaka 1994 ulipotoka tu.

Wenzetu wa nje wanathamini sana KAZI za Sanaa zao, wiki ya kwanza sokoni huo mkanda wa video (VHS) ulikuwa bei sana, nikajifunga kibwebwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…