Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Jopo la washauri bingwa la Afrika Kusini Ichikowitz Family Foundation hivi karibuni imetoa “Ripoti ya Uchunguzi wa Vijana wa Afrika (mwaka 2024)”, ambayo liliwahoji zaidi ya vijana 5,600 wenye umri wa miaka 18 hadi 24 katika nchi 16 za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Ethiopia, Kenya na Tanzania. Matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa, asilimia 82 ya waliohojiwa wanaamini kuwa ushawishi wa China katika bara la Afrika ni chanya.
Gazeti la Marekani Bloomberg News limenukuu ripoti hiyo likisema bidhaa zenye ubora wa juu na bei nafuu za China na uwekezaji mkubwa wa China katika miundombinu barani Afrika ni “sababu kuu” ya matokeo hayo. Ikilinganishwa na uchunguzi uliofanywa mwaka 2022, ushawishi wa China na Marekani barani Afrika wote umeongezeka, lakini ikilinganishwa na China, Marekani na nchi za Ulaya bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika majaribio yao ya kuwa karibu tena na nchi za Afrika baada ya kuzipuuza kwa miaka mingi.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwaka 2000, China imezisaidia nchi nyingi za Afrika kujenga miundombinu kuanzia vituo vya umeme hadi barabara katika miongo miwili iliyopita. Nchi za Magharibi kwa sasa zinafikiria kujenga upya uhusiano na Afrika, ili kupata maliasili zenye thamani na soko kubwa barani humo. Huu ndio wasiwasi mkubwa zaidi wa vijana wengi wa Afrika ambao hawataki nchi zao zinyonywe na makampuni ya kigeni, hasa kuchukua maliasili bila manufaa yoyote kwa watu wa Afrika.
Je, kwa nini China ina ushawishi mkubwa zaidi barai Afrika? Labda Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCA) linaweza kujibu swali hili. Mkutano wa Mwaka 2024 wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umeanza Septemba 4 na unatarajiwa kukamilika Septemba 6 mjini Beijing, China. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kushirikiana ili kutimiza usasa, na kujenga jumuiya ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.” Viongozi wa nchi 53 za Afrika na Umoja wa Afrika wamehudhuria mkutano huo ili kujadili na viongozi wa China kuhusu mipango ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, kuchora ramani ya pamoja ya maendeleo, na kufungua ukurasa mpya katika ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.
Kwenye mkutano huo, rais Xi Jinping wa China ametangaza kuinua uhusiano kati ya China na nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kibalozi na China kuwa uhusiano wa kimkakati, na kuinua uhusiano kati ya China na Afrika kuwa jumuiya yenye hatma ya pamoja kwa siku zote katika zama mpya.
China ndiyo nchi kubwa zaidi inayoendelea, na Afrika ndilo bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea. China siku zote inazingatia ushirikiano wa kirafiki na nchi za Afrika kama msingi muhimu wa sera yake ya kidiplomasi. China na nchi za Afrika zitauchukua Mkutano wa Mwaka 2024 wa Kilele wa FOCAC kama fursa ya kuendeleza zaidi ushirikiano wao.