LutahNahshon
New Member
- Aug 1, 2021
- 1
- 6
Habari hivi ulishawahi kujiuliza ni kwanini vijana wengi wanaona maisha magumu sana katika karne hii ya 21? Majibu yote yapo hapa kwa kiasi chake.
Kwa kawaida kijana anahesabika kuanzia umri wa miaka 15-45 hao wote wapo kwenye kundi la vijana wananguvu za kufanya kazi na kuleta mabadiliko katika jamii. Lakini kwa nchi yetu vijana ndio wamekua wahanga wa kubwa wa umasikini uliopitiliza kwasababu zifuatazo kwa mujibu wangu
1.Uvivu,
Vijana wengi wanasubiri fursa ziwafuate nyumbani walipo hawaumizi kichwa kuangalia ni changamoto gani zipo kwenye jamii ili wazibadilishe kuwa fursa na kujiletea maendeleo binafsi na jamii kwa ujumla.
2.Elimu,
Vijana wengi hasa waliopata elimu wanapenda kuchagua kazi na kujikita katika kutafuta kazi kutokana na walichosomea tu hawataki kufikiria nje ya degree yake wengi wanafikiria kuajiliwa ofisin walipwe mishahara mizur bila kuzingatia kwa muda huu wasomi ni wengi na nafasi za ajira ni chache kwa hiyo lazma kila mtu afikirie kujiajiri kabla hata ya kumaliza masomo.
3.Uoga wa kuthubutu,
Vijana waliowengi wanaogopa kufanya kitu kwa kuangalia jamii itamchukuliaje au watu wake wa karibu kitu kinachomfanya kubaki akitamani kufanya kitu lakini uoga unakua kikwazo mfano kulima na ufugaji ni kitu kinacholipa lakini vijana wengi hawapendi hizo kazi za kuchafuka na kutumia muda mrefu.
4.Utegemezi,
Vijana wengi wanataka familia zao ndio ziwashike mkono ili waanze kufanya kitu ambapo sio sahihi kwasababu unafanya kwa ajiri yako na sio familia acha utegemezi uende mbele kama kijana lazima tujifunze kujitegemea usisubiri kila mtu akupe kitufulani au akuunge mkono ndio uanze biashara anza wewe kama wewe usimuangalie mtu.
5.Serikali,
Kumekuepo na malalamiko mengi kutoka kwa vijana kwenda serikalini kwamba haisaidii vijana mara hili mara lile lakini kama kijana wa kitanzania hebu fikiria wapo vijana wangapi tanzania je serikali inaweza kumpa mtaji kila mtu?? Haiwezekani kwahyo tuache kuitegemea serikali sana katika kujiinua kiuchumi kikubwa miundombinu ipo na kuna uhuru wa mtu kufanya biashara bila kuvunja sheria tuanzie hapo tusisubiri serikali kutufanyia kila kitu.
Sasa tuone ni kitu gani tunaweza fanya kama vijana kujikwamua kiuchumi,kijamii na kimaendeleo kiujumla
1.Kujifunza,
Kama kijana inatupasa kukubali kujifunza kila siku ili kupanua uwezo wetu wa kufikiri na kuwa na mawazo mengi na njia nyingi za kujikwamua kiuchumi tusome vitabu,majarida na kusikiliza vipindi vya vijana katika redio na televisheni
2.Kuvumilia,
Kama kijana hutakiwi kukata tamaa kirahisi hasa unapoanzisha kitu jitumee na usikubali kurudi nyuma hata sikumoja kila kosa liwe funzo kwako kufanya kwa ubora zaidi ishi katika kile unachokiamani.
3.Muda,
Kijana tumia muda wako vizuri maana huu muda tunanguvu za kufanya kazi acha tufanye kazi kweli kwa ajiri ya maendeleo yetu na jamii kiujumla kila muda uwe ni wathamani kwako usipoteze muda kwa sababu haujirudii.
Mwisho mshirikishe mungu kwa kila jambo unalolifanya ukiamini unaweza na mabadiliko yanaanza na wewe naamini kwa pamoja tunaweza kubadilishi imani mbaya ya watu wengi kuhusu vijana muda wa mabadiliko ni sasa kwa pamoja Tunaweza.

Upvote
6