jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Hili swali huwa najiuliza sana.
Mara zote ambapo vita ya dunia ilitokea, sababu kubwa unakuta ni maslahi ya mataifa makubwa. Mataifa ambayo yanapishana “ideology”
Mfano mataifa ya mashariki na magharibi. Na inakuwa vita ya dunia kwasababu utakuta kila nchi ina upande iliyochaguwa hata kama siyo kwa wazi. Na athari za vita ni kila bara linaathirika kwa namna moja ama nyingine…either directly or indirectly.
Kwenye hili suala la vita vya mashariki ya kati, kuna maslahi ya mataifa makubwa. Lakini maslahi hayo yako “intertwined” na masuala ya kiimani. Ambapo yanapewa uzito sana na mataifa hayo.
Pamoja na kwamba ideologies za capitalism na communism zilitaka kusababisha vita ya dunia hadi kuingia kwenye “vita baridi” baina ya mataifa hayo makubwa, bado mataifa hayo ikija kwenye imani wanakuwa wanakubaliana mambo mengi.
Hata wakomunisti wengine ni wakristo. Only wachina ndo tofauti. Lakini ubepari, wenyewe umejikita kwenye ukristo kiasi cha kwamba mataifa hayo yakaona kuwa ukomunisti ni adui mkubwa kabisa wa “western civilization”
Vita vya Middle East navyo viko kiimani zaidi. Lakini hakuna wakomunisti wanaokubali kujitolea kuwa upande wa watu wa Middle East ambao ni waarabu na waislam.
Hata Russia mwenyewe anasuasua na kuchagua wa kusaidia. Mfano Saddam na Ghaddafi walifumba macho NATO na Marekani wakachinja wanavyotaka.
Lakini kidogo kwa Iran na Syria amewasaidia lakini siyo “full support” mfano anayoifanya marekani kwa Israel. Ambapo marekani yupo tayari kabisa kuingia vitani kumsaidia Israel.
Lakini pia naona marekani ameshakubaliwa sana kuingiza maslahi yake mashariki ya kati. Na hata kuweka uongozi ambao ni vibaraka wake. Na kule kuna kambi zao nyingi za kutosha za majeshi.
Marekani wana mfuta, lakini hawachimbi. Wanakunywa Middle East huko kwa waarabu. Hata pale Saudi Arabia, familia kubwa ya kitajiri ambayo ndo familia iliyoijenga Saudi Arabia, familia ya Bin Laden, yule Osama alifanikiwa sana kupata sapoti ya waarabu wengi ambao hawakuwa wamefurahishwa na uwepo mkubwa wa wamarekani kule Saudia. Na pia marekani waliingia mikataba na familia ya kifalme ya Saudi, kwamba marekani apate mafuta, na yeye Msaudi apate ulinzi na silaha kutoka kwa mmarekani.
Kwahiyo sababu za wamarekani kuacha kuchimba mafuta yao, ni mambo ya “timing”, pia msemo wao wa “adui muweke karibu”
Mfano wao wa Saudi, uoga wao na tamaa za kubakia madarakani, ndizo zimesababisha vita huko kwao isiongezeke na kuwa vita kuu ya dunia.
Leo hii wangewanyima wamarekani mafuta, kuna uwezekano mkubwa vita ikawa ya dunia.
Kwa upande mwingine, China na yeye yupo kimya kwasababu mbali mbali. Ambapo huwa anatoa kauli za kulaani, lakini hakuna hatua yoyote.
Hata wakina Kiduku huwa hawaoni kama vinawahusu. Kiduku amemsaidia Putin dhidi ya Ukraine, lakini sijawahi kuona wala kusikia aki “sympathize” na dhahma ya mashariki ya kati.
Naomba wenye maoni tupeane hapa. Ni kwanini hivi vita ni kama vile “Mambo ya Ngoswe”?