Pendo lililobarikiwa MM,
Natambua ni usadikifu wa wengi kuwa kuna Mungu japo uwengi wao haufanyi hilo kuwa ni hivyo hasa...
Nimezipenda mno hizo picha ulizochagua na kuambatanishia swali--kama kawaida, zimeikiwa kwenye kasha langu la picha mbalimbali... Kwangu huwa zinaamsha mambo mengine hata ya mbali na sayari ya dunia; japo nikikaza mawazo yangu kwa mambo ya hapa kwenye dunia yetu ninafurahia sana uzuri na urembo ajabu wa viumbe anuai katika sayari moja...
Mwanzo na mfanyiko wa viumbe vyote ni utukufu na sifa ya ua ndani ya ua... Ninazungumza kiushairi lakini kiufundi ukweli wa mambo ndivyo ulivyo; katika ulimwengu wote mzima na katika sura ya yaliyodhahiri na yasiyodhahiri, uzuri na urembo ni ishara ya uakili usiokifani na ishara ya nekta, mguso laini na hata manukato ya uhalisia unafutika mwingine--na yote kuwa basi mfano moja kuwa ndani ya mwenzake pasipo nukta ya kiini wala mzingo wa mapana... Ulimwengu uliodhahiri hauna mwanzo wala mwisho, na kama ilivyo ndani ndivyo ilivyo nje. Ilivyochini ndivyo ilivyo juu...
Viumbe hai vyote hufanyika kuwa na halafu humong'onyoka kwa kanuni zenye kufuatisha sifa ya utukufu wa hata kile tusichokiona kwa macho... Hicho chaweza kuwa ni 'Yabisi' kabisa katika ulimwengu wa namna yake lakini usioingiliana na miguso ya fahamu zetu za kawaida. Basi japo wengi katika hali ya kawaida hupenda kutazama sura ya mambo kwa kule kusema kitu 'kiliumbwa'--katika huu ulimwengu hakuna kitu kama kuumbwa hasa... Kuna 'uumbajikaji'--na huu upo wakati wote; daima umekuwa--milele unakuwa. Kila kifanyikacho kuwa dhahiri kwa muktadha, hali na picha fulani kwa namna ingine chaweza kuwa ni sehemu ya sifa yenye mapana marefu kuliko tuwezavyokumaizi kwa wakati. Ni kwa jinsi hii kidogo tu, watu wa visomo vya historia vya viumbe na masalia huleta zile nosha za ukuwakujia--evolution. hawa hupatia patia ukweli wa mambo wanavyozungumzia nasibu ya viumbe kubadilika katika vipindi virefu vya nyakati ili kupatia sura iliyobora kwa uzima na ustawi wa kiumbe lakini mengi wanayozungumza mpaka sasa ni nusu ya simulizi kwa kuwa nusu yake haijapata kusimuliwa...
Ulimwengu wote ni maua, haya huja kwa kanuni za uzima, kheri na utangamano uliofichika wa maumbo na uweza wa nguvu usiokoma nguvu. Nifupishe simulizi la kutanua mashauri ya msuko wa miili hai na ile isiyo hai ndani na muktadha usioonekana wa uhai kwa kudodosea jambo... Kadiri ya kufanyika kwa yote ni fumbo na hapo hapo ufunguo kwa siri za uzima. Wewe umevutiwa na macho, basi nitakuambia jambo... Macho mawili ya viumbe hufanyika hivi kwa kuwa kila mwili wa kiumbe ufanyikao kwa mapana ya sehemu ya 'uyabisi' usiodhahirika wa ua letu la uzima na tena wenye kutia uzima na maana ya maumbo na mienendo ya uzima huhifadhi neno kwa simetria ya unusu na unusu wa jinsi ya kiume na kike katika kila mwili wenye kuhaika... Lakini unusu huu pia hufungamana na siri za (1)damu za hisia ilivyo ni muktadha tiririvu na (2)miundo tuli ilivyo ni sura ya usimamivu na uyabisi wa maumbo hata yale yenye uhai.
Kuna siri katika hisia kwa maana ya kile ambacho mashauri ya kiingereza hutajwa ni 'Emotions' na ni dhumuni kuja kutafutia neno muafaka kwa hisia kwa muktadha kama hatua maandalizi ya kisomo rasmi cha ufunuo wa siri za maumbo yenye kunyambulika kiuhai. Hisia kwa namna ya neno hili 'emotions' ni kipitisho cha usumaku wa maumbo hata kwa mapana ya kweli tusizozielewa vizuri kwa sayansi yetu ya leo... Azma yangu sehemu ya kweli hizi tutazichimbua na zitatuleta uwezo hata wa ajabu katika ujuzi na maarifa juu ya siri za viumbe hai na uzima uliohifadhika--hii pia itakuwa ni kufunguo kwa tiba na uponyaji... Macho yanahusiana sana na akili, utambuzi na kujitambua kukidhi sifa maalum za kiumbe chenye hayo; tofauti ya kiumbe chenye macho na kile kisicho na macho ni kuwa mapana ya jaala ya kiumbe hata katika sura pana ya ukuwakujia yatakidhi sifa na hadhi tofauti katika ustawi wa kimazingira na kujitosheleza. Katika mapana ya hata mfumo wetu mkusanyiko wa majua--katika mpangilio wa falaki; nasibu ya viumbe hai vingi vinakadirisha hadhi ya fahamu tano za kimsingi--na ndivyo achitipu, kudra na hadhi za kiakili huchachuka katika kunasibu uzuri wa maumbo ya uzima kwa kujitahidi kutangamana na mawimbi ya hisia na kheri ya maumbo mapana zaidi ya falaki zilizodhahiri na kusema basi katika muktadha usiodhahiri wa ulimwengu tuutambuao...
Kadri unawezavyo kutambua siri za majimaji ya uzima wote umejua 1/3 ya mpango mzima... Ulimwengu kwa sifa na utukufu kamili ni 3/3 kote na mote.
Katika umajimaji huu vyote vyafanyika na milele yote... Usipotoke kamwe na vina vya tafsiri kwa udhanifu na nosha za mafikara ya kuendesha fikra ulizozizoea kwa mapelekeo ya uwezo na mazoea yake. Kuna upande mwingine wa mambo utaokubidi wewe kurudi kuwa kama mtoto mdogo na kukana unachofikiri unajua... Naam hata mafikara, usadikifu na imani isiyochujwa ili kuwa safi kuelekea kwenye hakika na kweli ya yote. Kwa kuwa kabla ya hapo, maombi yote kwa miujiza ya maisha ni kimvuli cha ujinga, laana ya tabu na kifungo cha hiyari katika uwanda wa kiza.
Kuelekea miujiza kamili na kuachana na jicho la mwili lenye kutenda kwa mafikara ya makusudio ya miili kwa neema isiyobayana kwake. Kufanya macho mawili kuwa moja kunaweza kukuingiza katika utambuzi wa kweli kuu kupita tafsiri za uzima wa maumbo kwa jinsi na kadri udhaniavyo... Kuyashinda macho ya mwili hadi kuelekea moja unakuwa katika 2/3 ya mpango mzima...
Itoshe kwa leo