Kiasi gani hutolewa? Kuwa muwazi!Habari zenu,
Nina ofisi zangu za Uwakala wa mitandao ya simu na nimekuwa nashangazwa na Kamisheni ndogo zinazotolewa na Vodacom.
Mitandao mengine ipo vizuri kiasi chake lakini Vodacom wamekuwa wanabana sana Commission kwenye miamala ya kuweka na kutoa.
Hii hali imeenda mbali zaidi kwani hata ukiuza Vocha za kurusha nako wanapunja Commission.
TATIZO NI NINI?
Kuna miamala unayofanya lakini haina kamisheni ,
Mfano kuweka au kutoa pesa mtu akiwa mbali.
Unaletewa namba na mteja kwenye kikaratasi unaweka hela , hapo hakuna kamisheni