Kwanini vodacom wana bei sana kwenye vifurushi vyao?

nyanga kante

Member
Joined
Jan 7, 2017
Posts
36
Reaction score
34
Kwa mnao faham naombeni mnisaidie kuusu hili. Kwanini vifurushi vya Vodacom vina bei sana tofauti na mitandao mingine kama Tigo, Airtel...... Ni kwamba vodacom wameridhika sana na wateja wengi walio nao au imekaaje hii. Watalam wa mambo nawaomba mnisaidie
 
Wapandisha bei ovyo ovyo sana
 
Jibu ni kwamba maisha yanabadilika..Gharama kila mahali hata dala dala tulianza tumia nauli sh.30
 
Yamepunguza mbs arafu yanatuma msg kwamba yameboresha vifurushi.. [emoji2959] Sana
 
Udhaifu wa competitors wa voda ndo unaosababisha voda watunyanyase
 
Voda ndo baba lao nadhani technologia yao iko imara zaidi ndo mana mara nyingi voda ktk huduma zao hawazingui text, call, internet vyote vipo stable ukicompare na wengine
 
Voda naitumia kwa masuala ya kifedha pekee lakini kwa mambo ya vifurushi siitumii kabisa, hivi kweli kabisa 1000, mb 200 si masiala haya wakati nikijiunga na ofa ya halopesa bando napata mb 500 kwa sh. 500.
 
Wewe kwanini ulinunua line yao huku ukijua ni ghali?
 
wana huduma nzuri sio wez kama tigo yaan ata uweke salio bla kujiunga likakaa siku nzma basi utalikuta mlad ujawasha data wala ujapiga cm ila sio kwa tigo..kifupi ndo mtandao unaoongoza TZ adi vijijin.
 
nimechungulia vifurushi leo nimekuta cha shilingi 2500 wamepunguza MB kutoka 1500 mpaka 800MB
 
Ifanye laini ya voda kama bank.


Ifanye laini ya Tigo/halotel kama suluhu ya kuingia internet
 
Aise me naona huyu MD mpya WA VODA ni mbovu sana. Tangu aingie yeye ndo vifurushi tunaibiwa balaa, mimi personally nimeibiwa vifurushi nimelalamika wee hamna msaaada. Uozo starts from the top, mbona mwaka jana haikua hivi? Au ni mimi mwenyewe? Siku ya leo zimeenda 10GB ndani ya lisaaa sijui zimeishaje...nimeenda mpaka vodashop yani hamna msaada, yani siku nikikaa vizuri hii kesi naipeleka mahakamani nina hamu za million 60 za kumfungulia mamaa duka la nguo maana imekuwa kero sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…