Pre GE2025 Kwanini vyama vya siasa kila siku ni katiba mpya na ununuzi wa ndege? Athari za mabadiliko ya nchi kwanini hamzipi vipaumbele?

Pre GE2025 Kwanini vyama vya siasa kila siku ni katiba mpya na ununuzi wa ndege? Athari za mabadiliko ya nchi kwanini hamzipi vipaumbele?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Uchaguzi umekaribia. Tunajua CHADEMA watakuja na sera zao Katiba mpya meanwhile CCM watakuja na sera zao za jinsi walivyonunua madege, kujenga flyover na SGR.

Lakini kwanini, vyama hivi havizungumzii kuhusu masuala ya utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi?

Mvua za El Nino, ukame na mafuriko ni mambo ambayo wananchi yanatuathiri sana lakini kikija kipindi cha uchaguzi viongozi wa vyama vya siasa wapo kimya wanang'ang'ania katiba na ujenzi wa mabarabara.

Kila siku sera na ilani zao ni zile zile.

Ukiangalia ilani za vyama vingi vya siasa, CHADEMA kwa mfano, kwenye ilani yao, mambo ya mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi hawajaweka kwenye vile vipaumbele vyao 20.

Soma Pia: Tanzania inaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

CCM ndo kabisa. Utunzaji wa mazingira wameeka kwenye kipengele walichokiita Mengineyo.

Kwanini wanasiasa wetu hawaongelei mambo haya kwenye majukwaa ya uchaguzi? Kila siku ni mambo ya madege na katiba mpya? Au hawaoni jinsi mvua za El Nino zilivyotuathiri mwaka huu?

Mimi nashindwa kuwaelewa kabisa wana shida gani.

Nawasilisha
 
Hata kabla hujaandika hapa,ajenda ya Nishati safi imebebwa na Rais Samia na aliizindua Toka mwaka juzi.

Kwa Sasa kinachoendelea ni utekelezaji kama hivi 👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/C_3JbCTtsp1/?igsh=Zmt0aTIxeDMzM2N3

Hao wengine ajenda zao kuu Huwa ni maandamano 😂😂


Nishati safi sawa lakini bei yake mimi mtanzania wa kawaida naweza kuimudu?

Watanzania tuko Milioni 60 lakini mitungi ya gesi inayotumika nchini ni 400,00 tu.

Kweli unaona hapo kuna kipaumbele mkuu
 
Nishati safi sawa lakini bei yake mimi mtanzania wa kawaida naweza kuimudu?

Watanzania tuko Milioni 60 lakini mitungi ya gesi inayotumika nchini ni 400,00 tu.

Kweli unaona hapo kuna kipaumbele mkuu
Umesoma hiyo link? Lengo lake ni kuweka ruzuku Ili mtungi complete upatikane Kwa 25,000 ule mdogo Ukiwa na jiko lake na gesi ndani badala ya 65,000 nk nk
 
Back
Top Bottom