Asante sana kwa kushare andiko hili. Utawala unaojiita wa kidemokrasia huku ukiwa sio, ni mzizi wa udanganyifu kwenye kila sekta ya maisha yetu.
Sasa sababu unafaidika na utazidi kufaidika na ujinga na habari nyenyepesi kuhusu watu wake huku mzizi wa yote hayo ni mkubwa sana hakuna ambae anayeweza kuthubutu kupambana nao kuutoa sababu kila mmoja alishawahi kushiriki, hivo wanabaki kuuendeleza hivo hivo japo wana maumivu makubwa huku wakistaafu wakitamani wangekua na guts za kufanya kitu flani kwa taifa lao. CCM unlike CCP in china haijawekeza kwenye technology na nguvu zao za utawala wamekeza kwenye cheap propaganda na ujinga wa jamii yetu kitu ambacho sio endelevu. CCM inabidi iwekeze kwenye Elimu na Technology japo ikiwadhuru wao lakini kwa faida ya Taifa letu. Elimu,Elimu,Elimu.
Mimi siamini katika Demokrsia ya Kitapeli inayofanywa na watawala wa Afrika .
Haitatufikisha mbali zaidi ya kuurudisha Ukoloni kwa mgongo wa nyuma huku wao wakijiwekea sheria za kujitajirisha wao na familia zao kwa vizazi na vizazi .
Hata ulaya na Marekani haikuingia kwenye Demokrsia kitapeli . Walitokea watu wanaoamini na kuiiishi demokrasia ndio wakaleta mapinduzi ya kisiasa .
Kama hatuwezi kupigania demokrasia ya kweli tukamweka madarakani mtu kama Tundu Lisu anayeamini katika Demokrsia basi ni bora pasiwe na huu ujinga wa Demokrasia yenye Raia wanaoamrisha Jeshi kutumia mabavu dhidi ya wananchi wake .
Yaani unakua na chama Tawala kinachopandikiza wanajeshi makada kwa ajili ya kupambana na wapinzani. Hii ni hatari sana maana panakua na kufitiniana ndani kwa 'ndani kwenye vyombo vya dola . Matokeo yake ni kujipendekeza kwa kufanya ubaya badala ya kusimamia majukumu ya vyombo hivyo .Wale wanaoonekana kutorudhishwa na mfumo huo wanafinywa kimya kimya matokeo yake ni udumavu mkubwa wa Demokrasia
Sasa kwa nini tuwe na matumaini ya kupata demokrasia kwenye mfumo wa kijeshi unaojivika koti la demokrasia huku yanayofanyika ni mabaya zaidi ya nchi za kijeshi.
Uganda sio nchi ya Kijeshi ni nchi ya kiraia na kidemokrasia ya vyama vingi .
Rwanda sio nchi ya kijeshi ni nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi kama ilivyo Tanzania.
Zote Rwanda ,Uganda na Tanzania zinafanya chaguzi za maigizo huku ziki poteza fedha nyingi bila sababu. Kama wanajua kuwa hawataki kushindwa basi wasipoteze pesa za umma kufanya uchaguzi .
Teknolojia ni kipaji kinachoweza kutokea popote kwa sababu inafumula zake . Kinachotakiwa ni uwekezaji na kuwatumia wataalam wa ndani.
Hivi kiwanda cha Tairi kilikufa kwa sababu ya teknolojia au usimamizi mbovu ?
Kiwanda cha viberiti kilikufa kwa sababu ya nini ?
Je ,CCM inajua tu kupambana na akina Dr. Slaa lakini sio wezi wa mali za umma ?
Kiwanda cha Tan bond kilikufaje wakati wasomi wakiwa wachache kilifanya kazi ,wasomi na soko limekua kubwa kiwanda kinakufa .
Watawala wanashirikiana na wawekezaji kutoka nje kuua mali za umma.
Tulikua na kiwanda cha redio ,kiwanda cha baiskeli cha swala. Kiwanda cha kuunganisha magari ya Scania . Kiwanda cha Jeshi cha Nyumbu cha kutengeneza magari . Kiwanda cha nyama kinakufa wakati soko linaongezeka .
Kilifanya kazi soko likiwa
Mwafrika unakuta mzazi anapiga mtoto viboko au makofi kisa anacheza
Akirudi mchafu anapigwa kama kibaka
Akifeli mtihani anapigwa haswa ila hasaidiwi makosa yake ila ni kudunda tu
Hiyo nidhamu unayoisema ni ipi hapo?
Mtoto mdogo anahitaji msaada mkubwa sana wa kujua mabaya na mazuri kwa kusimamiwa na kufundishwa
Mzazi anakuwa adui mkubwa wa mtoto sasa wizi utakosekanaje hapo
Ukiwa adui na mtoto atafanya mabaya yote akijua ndio furaha yake
Wazazi lazima tuwe na ukaribu na watoto na kuwafundisha mema na kuwalataza mabaya
Mzazi ana matusi balaa kila dogo akifanya kosa ni matusi na kipigo
Halafu mnaita eti nidhamu
Hiyo sio nidhamu bali ni ujinga wa baadhi ya wazazi na hawajui malezi
Mtoto ni lazima acheze na wewe kama mzazi mwangalie na huku ukimuonya hatari zinazoweza kutokea
Watoto haohao walikua wanakua walimu na makisi . Kama sio neema ya Mungu basi wanakua walimu katili sana na mapolisi katili sana .
Mwalimu anamchapa mwanafunzi kwa hasira na wakati mwingine anakua na chuki kabisa na mwanafunzi tena wa Nursary . Wanafunzi nao wangekuwa kuwa wahalifu wakiwa shuleni .
Mfano shule nyingi za boding za serikali ,wanafunzi hasa wa kidato cha nne wakimaliza shule wanaharibu miundo mbinu ya shule .Wanavunja taa za umeme ,wanavunja vioo,wanavunja ,koki za bomba ,wanavunja swichi na kufanya fujo nyingi .Yaani wanakosa malezi ya kupenda mali ya umma. Na walimu wanashindwa kuwaandaa kwa kuwafundisha umuhimu wa Kulinda na kuthamini mali za umma.
Siku hizi kila idara watu ni waoga wa kutaja neno haki na uzalendo.
Yaani mwalimu alitaja uzalendo anaonekana ni mpinzani /Chadema hivyo ni rahisi kushughulikiwa maana walimu wengi wamekua machawa hasa wale wenye elimu kubwa zaidi . Yaani kama ni shule ya msingi akishapata kadiploma au kadigrii anageuka kuwa Chawa ili mambo yake yaende.
Mwalimu akichaguliwa kuwa Mjumbe wa CWT anageuka kuwa Kada ili akila pesa za chama cha walimu asiguswe na ukihoji sana wanakuchongea wewe ni Chadema.
Hali kadhali ndani ya Polisi na vyombo vingine vyote vya Dola mpaka mahakama . Ukizungumzia haki na uzalendo unaitwa mpinzani . Yaani CCM haipo tena kwa ajili ya kusimamia sheria na haki katika nchi hii .
CCM imetekwa na genge la wahalifu wenye silaha kama basi linavyoweza kutekwa na majambazi .
Basi lilitekwa na majambazi hata wakisema vua nguo mbele ya mama mkwe na baba mkwe inabidi uvue na ukikataa wanakuua . CCM imetekwa na genge la mafisadi wachache ambao wanalindana na wanashindana kujilimbikizia mali . Yaani kuna familia sasa zinashindana kujilimbikizia mali kupitia fedha za umma . Na hao sasa wanamtumia De.Samia kama mlinzi wao kwa sababu ana majeshi nyuma yake na mahakama inaogopa kutoa haki maana ukizungumzia haki basi wewe ni Chadema .
Ndio maana leo wakristo wote wanaonekana ni Chadema kwa sababu wito mkubwa wa ukristo ni kutenda haki na kuwa na kiasi , Kutoa kodi kwa haki , kupenda wengine kama nafsi yako ,kuwatendea wengine kile ambacho wewe unakipenda utendewe na kufurahia uhuru ndani ya Kristo . Sasa Maaskofu na wachungaji wa kweli wanaonekana ni Chadema kwa sababu wanhubiri injili inayozungumzia Haki . Waislam wale wenye jitihada zao binafsi za kujitafutia riziki na uwezo wa kupambanua mambo na kusimama kwenye Ukweli uliopo ndani ya Quran na hadithi za mtume nao pia wamekua wakipigwa vita na hata kuawa kama Ally Kibao kwa sababu tu wanasema Ukweli kuwa Uislama kwa karne nyingi ulipigania Haki ya waarabu mpaka wakajikomboa . Lakini kinachotokea ni CCM kutekwa na matajiri waotoa rushwa na mapesa mengi kwenye nyumba za ibada na kujenga nyumba za ibada.
Mbaya zaidi ni kutafsiri vibaya sadaka zinazotolewa na fedha chafu kuwa zinafuta dhambi zote .
Kama ni kweli kuwa sadaka zinafuta dhambi zote basi tuseme chini ya CCM Tanzania inaangamia kwa kasi kubwa sana.
Magaidi hua wanatengenezwa na genge la matajiri ndani ya mifumo . Haya tuliyaona awamu ya Nne wakati JK anakaribia kumaliza Muda wake . Ugaidi ulipamba Moto mpaka Jeshi la Wananchi kushirikiana na vikosi maalum vya polisi vikaingilia kuwasaka baada ya Magufuli kuingia . Ina maana kuwa kama JPM angezubaa nchi ingegawanyika na isibgetawalika wakati huo huo kuna watu walikua wanapewa matrilon ya pesa toka Uarabuni kwa sababu ya kuivuruga nchi ndio maana JPM alizuia pesa zote kutoka nje ili magaidi wakose wadhamini na misaada . Majeshi yetu chini ya Mzalendo Magufuli wakafanikiwa kuwaondoa magaidi mengine yakakimbilia Msumbiji. Genge lao liliojaribu kuingiza nchi kwenye ugaidi wengi wapo sasa na wameinua mikia juu kwa furaha kuu. Vyombo vya dola vikiichekea hii CCM isiyotaka uchaguzi wa kura vitakuja kupata kazi kubwa sana huko mbeleni kwa sababu CCM haijali tena ustawi wa nchi zaidi ya kujichotea mali za umma .
Jeshi na polisi wamekaa kimya Bandari zinauzwa kwa Watu ambao kwa historia waliwahi kugawana rasilimali zetu kwa damu za watu na kuzifanya kuwa zao kwa ajili ya kujitajirisha.
Kama karne kumi na mbili zilizopita waarabu waliwaza kuja kuchukua Pembe za ndovu na dhahabu na mbao Tanganyika leo karne ya ishiri na moja unategemea lile wazo limepotea ?
Bila shaka waarabu hawakuondoka Tanganyika kwa kupenda bali waliondoka baada ya uhuru . Mbaya zaidi wana ndugu wengi humu wanaotumika sasa kuhujumu nchi.
Hata kwenye mitandoa kuna wahuni wengi na machawa wengi wenye asili ya kigeni kazi yao ni kujenga chuki na kutukana watu matusi makubwa sana . Wanamtulaka mpaka baba wa Taifa aliyeanzisha Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa heshima kubwa . Aliyeanzisha Usalama wa Taifa kwa heshima kubwa . Aliyelinda rasilimali za nchi hii kwa ajili ya vizazi vyetu kwa heshima kubwa . Leo wametokea wahuni wanamtukana Nyerere ,wanawatukana maaskofu , wanawatukana Wanaharakati na kuwatukana watu wote wanaozungumzia habari ya haki ,uhuru,utu,umoja na mshikamano wetu uliokuwepo ,uzalendo na ulinzi wa rasilimali zetu.
Chaa ajabu hao wahuni hawakamatwi bali anayakamatwa na kunyanyaswa ni Dr. Slaa .
Unaachia magaidi yaliyochoma moto makanisa Zanzibar na kuua mapadri na kuwamwagia tindikali halafu unamfunga Padri Slaa anayeonya kuhusu ufisadi unaofanywa na wahuni kwenye nchi yetu . Inawezekana yale magaidi ndiyo yamegeuka kuwa machawa mitandoani .