Kwanini waandishi wa simulizi wa bongo huweka kazi zao mitandaoni bure?

Kwanini waandishi wa simulizi wa bongo huweka kazi zao mitandaoni bure?

AK Mastori

Member
Joined
Jul 26, 2024
Posts
5
Reaction score
6
Habari wakuu. Ni swali tu nimejiuliza hili. Kuna kazi nyingi sana za waandishi ambazo zipo tu hata huku JF, tunazisoma bila ya wao kufaidika chochote. Natafuta lengo la kufanya hivo lakini kila ninalowaza halileti mantiki, lenye mantiki ni labda wanatoa sadaka kwa namna hii. Kwa wale waandishi, nina shauku ya kujua mnafaidika vipi na kutoa kazi yako bure.
 
Hiyo ni aina ya matangazo. Umeisoma ulianza kunogewa, hapo Sasa anaanza kukwambia jiunge whatsup group kwa 3000 usome vipande vyote. Alipata watu 200 ana 600000...hapo ni kiwango Cha chin Cha elfu tatu.
Huko YouTube alipata views nyingi analipwa na youtube
 
Lakini shida ni kwamba kazi ukishaiweka hivyo kila mtu anakwambia ni yake. Unakuta stori moja ipo magroup 10. Bado chances za mtunzi kufaidika zinakua ndogo sana.
 
huwa tunawapatia demo tu. ila lengo tunatafuta wasomaji wapya. maana kutokea hapa nimepata heshima ya Kimataifa. Kama nisingeliweka kazi zangu hapa nani angelifaham kama nipo ulimwengu huu?
 
Back
Top Bottom