Kwanini wabongo wanadhani kutafuta mpenzi mtandaoni ni umalaya?

Kwanini wabongo wanadhani kutafuta mpenzi mtandaoni ni umalaya?

Mdudu Mende

Member
Joined
Mar 31, 2021
Posts
78
Reaction score
120
Mpenzi huweza kupatikana mahali popote iwe klabu, kwenye ngoma, shule, kanisani nk. Ni suala la kupatana tu. Kuna watu wanakesha makanisani na hawapati watu wa kuwa nao na kuna watu wamepatana barabarani na wamedumu.

Ukuaji wa teknolojia umefanya zoezi la kutafuta wapenzi kuwa rahisi kwa kuwa na dating sites au vipande vya kutafuta marafiki, zamani kulikuwa na pen pals ambao ilikuwa unaweza kuwatafuta kwenye magazeti.

Dating sites za wenzetu zimeweka vigezo vingi sana ikiwemo rangi, shape, kama mtu ni mnywaji au mvutaji na zimekuwa na matokeo chanya kwa watu kupata wanaoendana nao. Hapa JF kuna Love Connect ambayo ni mahususi kwa kujitafutia wapenzi, naona hali iko tofauti kwa kuwa hata mrejesho wa watu kupata wapenzi ni mdogo.

Dada mmoja hivi karibuni alileta mrejeshi kuwa wengi wanamuona malaya. Why is Tz this backward kwenye kujua kuwa unaweza kupata mtu serious kwenye mtandao na mkaenda vizuri.

Mind you, kwa sasa watu wana kazi nyingi na ni vigumu kukutana na watu hasa kwa wale ambao wako ofisini na hawana starehe, hivyo hawawezi kwenda klabu nk, mtandaoni ndio kunakuwa sehemu sahihi ya kupata wenzi ambao wanaweza kudumu nao.

Nadhani suala la kudhani mtu anayetafuta mpenzi mtandaoni ni malaya ni kutokubali mabadiliko ya teknolojia.
 
Fikira za wachana wengi wa bongo ni hivo, mpenz wa kujua mtandao ni malaya. 😂😃😃

Niujinga acheni,

Ila sababu kubwa ni kwakotokujiamini kwao, wasichana wanaojiamini karibia wote wakihitaji mahusiano hupata haraka sana.
 
Mkuu hizo ni opinion zao tu,, Wewe angalia target, then kwa muda wako endelea.......
 
Shida nikuwa Malaya wengi wa kibongo wamejazana kwenye hizo dating sites na profile zao zinaonesha wanatafta wachumba au mme na sio hookup lakin ukifata wanakwambia una sh ngapi. Hii imepelekea ata wale wachache wenye uhitaji kweli waonekane nao ni Malaya tu.
 
Hiki nilitaka kusema, nashukuru umenisemea na mm, n kwamba n ss wenyewe tunaoharibu hiyo mitandao
 
Mpenzi huweza kupatikana mahali popote iwe klabu, kwenye ngoma, shule, kanisani nk. Ni suala la kupatana tu. Kuna watu wanakesha makanisani na hawapati watu wa kuwa nao na kuna watu wamepatana barabarani na wamedumu.

Ukuaji wa teknolojia umefanya zoezi la kutafuta wapenzi kuwa rahisi kwa kuwa na dating sites au vipande vya kutafuta marafiki, zamani kulikuwa na
Ni culture na inahitaji muda kuzoeleka wengi wanafanya hii kwenye kucheat ila sio kujenga mahusiano makini japo kwenye kucheat inaweza geuka ila kila mmoja anaweza kuwa skeptical kwa mwenzake. Uhuni unafanywa kwa kutumia simu na mitandao usipime acha tu
 
Hiki nilitaka kusema , nashukuru umenisemea na mm, n kwamba n ss wenyewe tunaoharibu hiyo mitandao
Wenda na lugha inatuchanganya watu wanashindwa kuwa wawazi na kibaya zaidi site special kwaajiri ya hizo shughuri hazina members wengi kama site za dating
 
Back
Top Bottom