Binafsi sielewi kabisa sababu za Wabunge kupigania Majimbo yao yagawanywe ikiwa hatuna mfano bora wa maendeleo katika jimbo dogo.
Kwanza, Vigezo vyote vilivyowekwa ndani ya Katika ya JMT havilingani kabisa na Uhalisia maana Zanzibar kuna majimbo hayakidhi vigezo hivyo na sidhani kama Katiba ya Zanzibar inaruhusiwa kukinzana na Katiba ya JMT. Isitoshe hatuoni mafanikio zaidi katika majimbo madogo dhidi ya Makubwa.
Nachokiona hapa ni kwamba, nchi yetu Tumezalisha Wanasiasa wengi wachumia tumbo wakigombania nafasi chache zilizopo za Ubunge na sio hoja ya uwakilishi wa Wananchi maana Ubunge sio Udaktari wala Ualimu.
Siri iliyopo hapa, ili kukidhi haja zao wanataka tugawe majimbo mengine zaidi ili wapate nafasi zaidi za kugombea Ubunge kama kwamba Ubunge ni ajira.
Kugawa majimbo mengi zaidi haimaanishi hoja zitaongezeka ama mapato yataongezeka zaidi isipokuwa Matumizi ndio yatapanda wakati mfuko wa Taifa tulonao ni ule ule, hii itatugharimu zaidi haswa tukitazama gharama kubwa tunazotumia kuwalipa Wabunge hao magari, mafuta, mishahara, posho na mafao ya kustaafu.
Sidhani kama tunapogawa Majimbo zaidi husaidia zaidi kuwa na ufanisi katika ujenzi wa Taifa ama uwakilishi mzuri zaidi.
Uhalisia unatuonyesha kuna maendeleo zaidi katika Majimbo yenye watu wetu kuliko Majimbo yenye watu wachache hii inatokana na uwepo wa shughuli nyingi za Maendeleo kama vile kuwa na Mkoa, Wilaya, Jiji au manispaa na sii JIMBO.