Uchaguzi 2020 Kwanini Wabunge wazoefu wa Upinzani hawajaenguliwa?

Kwani wageni ni wapinzani peke yao, hakuna ccm mgeni uchaguzi huu?!

Mbona hawajaenguliwa ccm hata mmoja?!
Ccm wana utaratibu mzuri wa kusimamia ujazaji fomu wa wagombea wao ili kuepuka dosari.

Ila upinzani wameshindwa kuwasimamia wagombea wao wapya kujaza fomu kwa usahihi.

Kama hata kuwasimamia wagombea wao kujaza fomu kwa usahihi wameshindwa, je wanafaa kweli kuaminiwa na kupewa ruhusa ya kuunda serikali?
 
Hahaha ccm mijinga, Magufuli, Kabudi, Mpango, Ndalichako na PhD zao wanajaziwa form na mwanasheria?!

Yani ni nini kinahitaji mwanasheria kwenye ile form ya kugombea?!

Kujaza jina lako mgombea, anwaanibyako mgombea, taarifa zako binafsi mgombea, nazo unahitaji mwanasheria au kujaziwa?!

Ndio maana nchi inaongoxwa na wajinga kila siku malalamiko, kumbe hata form za kugombea hujaziwa?!
 
Wewe jamaa ni kilaza kweli sijui una njaa ya muda gani kichwani mwako?

Unaamini kwamba mgombea wa upinzani akijaza form peke yake ndo hajui Sheria.?
Inawezekana umesoma kichwa cha habari pekee na kuchangia au umechangia bila kuelewa ulichokisoma!
 
Reactions: RMC
Mbona sasa wagombea wenu wameshindwa kujaza hizo fomu? Ina maana wajinga wengi wapo upinzani ndio maana wao pekee ndio walioenguliwa.

Wagombea wenu kuenguliwa kwa kukosea kujaza fomu ni aibu kwenu.
 
CCM imeishiwa pumzi.kule pemba wamewaengua wagombea ubunge wote wa ACT sijui wanashindana na nani huko
 
Tatizo la wapinzani kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii lakini yanapokuja masuala ya muhimu hawaonekani au umakini unakosekana!
 

Hiyo ni calculated move ili kuonesha kuwa wameondolewa kihalali Kwani hufuatilii sababu zinazotamkwa za kuwaondoa na kuona kama siyo sababu za kutengeneza tumeona fomu ya gwajiboy kiapo cha maadili afamefanya tarehe 20/8 badala ya tarehe 25/8 siku ya uteuzi mbona hajaonfolewa. Hoja yako haina mantiki yoyote, kuna fomu ya mgombea wa CCM hajaisaini na hajaonfolewa ilikuwa humu kwenye mitandao. Ukweli unajulikana kwamba kuna nia ya kuitumbukiza nchi yetu kwenye machafuko. Mbona Haya mambo hayakuwepo wakati wa Mkapa na Kikwete hii awamu ni Mungu tu asaidie vinginevyo hii nchi itaingia kwenye machafuko sababu ya tume. Wote tuliona yaliyofanyika serikali za mitaa
 
CCM ilisambaza wanasheria nchi nzima kuwasaidia kujaza fomu .Upinzani kila mtu alikuwa akipambana kivyake

Walisambazwa wapi na hizo fomu zina kitu gani cha kuhitaji mwanasheria au hujaziona ukasoma hivi kundika jina lako la kwanza jina la Pili jina la ukoo na kazi yako kunahitaji mwanasheria kufanyanini. Awamu zingine mbona hatukuona haya wakati wa Mkapa na Kikwete. Tusidanganyane ati mwanasheria labda fomu za urahisi lakini siyo udiwani na ubunge
 

Nawewe unaamini kwamba kuna mbunge amekosea kujaza fomu basi utakuwa huelewi kinachoendelea katika hii nchi inamaana unanaamini kuwa wale wagombea wa serikali za mitaa walikosea kujaza fomu ndo wakaenguliwa karibia wote
 
Na yule mdada wa Morogoro! Si mzoefu?
 
CCM ilisambaza wanasheria nchi nzima kuwasaidia kujaza fomu .Upinzani kila mtu alikuwa akipambana kivyake

Sasa mdau mwenzangu wa Lumumba kama ni hivyo mbona mwenyekiti wetu wanamtuhumu kuweka picha ya pozi la aina yake?

Kama kwa mkubwa ilikuwa hivyo, je huko kwingine itakuwaje?
 
Naomba tume ya uchaguzi wahifadhi fomu za wagombea wote nchini. Itakuwa source ya data nzuri sana kwa ajili ya utafiti hapo baadaye. Bashiru na Kabudi watakuwa wadau wazuri sana ktk huo utafiti maana kwa kipindi kijacho hawatakuwa na majukumu ya kisiasa.
 
Kwahiyo mkuu wagombea wote wa CCM ni wazoefu hakuna mgombea mpya?
Ata kama tunalipwa kuongea ujinga na mapambio basi mengine tue tuna kaa kimya.
 
Reactions: RMC
Wamesaidiwa na wanasheria wa Chama kujaza fomu zao, Wakati Chadema ikiendelea na ule mchakato wa kusaka wadhamini, CCM Wao na vikao vya kujaza fomu n.k,

Ule Wakati wamejikalia kimya kumbe ndani yake kilikuwa kishindo, Uchaguzi ni mipango mkuu
Kama inawezekana tungeweka copy ya empty form hapa tuone kuna nini hadi wapinzani tu ndio wanakosea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…