Mzukulu
JF-Expert Member
- Feb 14, 2020
- 1,401
- 2,641
Wengi wao japo siyo wote hunywa sana Gongo na Pombe za Kienyeji ila sasa ni Wiki ya Tatu hii baadhi yao ninaowajua na ninaokuwa nao Maskani mbalimbali hawanywi tena Gongo na Pombe Chafu bali sasa wanakunywa Bia na pia wana Hela mno kiasi kwamba wapo wanaoniambia hata nikitaka Wanikopeshe Milioni wanaweza kwakuwa sasa Kimeeleweka.
Nikionana nao kila nikiwauliza kuwa kulikoni hivi sasa hawashikiki na wana Pesa na hawana muda wa Kupoteza Kunywa Gongo kama ilivyokuwa hapo awali wanabaki tu Kucheka na Kuniambia kuwa kwa sasa Soko lao limechanganya na kwamba nisitake Kujua zaidi ya hapo vinginevyo na Mimi watanichimbia langu wanifukie.
Na kama haitoshi pia wengi wao wanapata Wateja mbalimbali wa maeneo mengi ya Jiji ( Mji ) huu wa Dar es Salaam tofauti na ilivyokuwa au ilivyozoeleka. Je, kuna Mtu yoyote labda anaweza Kunielimisha kwanini Soko lao hawa Wachimba Makaburi limeongezeka ghafla na kwamba Siku hizi hawanywi kabisa Pombe Moto ya Gongo?