Huwa wanazuga hawataki kumbe wanataka. Kuna mmoja alikaribiswa kula akaringa kula kwa kuwa aliona mboga ni mlenda tu. Nyama zilipotengwa mezani akataka akaribishwe upya kwa kuwakumbusha wenyeji wake warudie kusema 'karibu tule', wenyeji wakarudia tena kumkaribisha jamaa akajaa mezani kula baada ya kuona kuna nyama. Wageni huwa wanazingua sana kula wanapoo chakula si kizuri na kitamu kwao. Kuna chakula huwa hakipishwi, mtu anajaa mwenyewe bila kukaribishwa na kuanza kula bila aibu. Nyama na tikiti halipishwi. Mnadani umejinunulia nyama choma yako vizuri imekatwakatwa vifanyango finyango umetengewa unakula kwa raha zako unashangaa wapitaji nao wanakaribia na kuanza kula bila kuwakaribisha na hawaoni aibu kuvamia meza.