Kwanini wagombea wengi Serikali za Mitaa ni Darasa la Saba na wenye uchumi wa chini?

Kwanini wagombea wengi Serikali za Mitaa ni Darasa la Saba na wenye uchumi wa chini?

Matulanya Mputa

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2023
Posts
245
Reaction score
655
Tuweke siasa pembeni, lakini ni mtazamo wangu kama nakosea mtasema.

Ukifuatilia wagombea wengi wa serikali za mitaa ni darasa la saba, au hawajasoma kabisa na watu wa kipato cha chini je serikali kwanini isibadili sifa za kugombea serikali za mitaa?

Sababu tukipata watu au wataalamu mbalimbali itatusaidia kwa namna moja ama nyingine.
 
Nini Job description ya Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa na Je hio inahitaji degree kuweza kufanya hayo anayotakiwa kuyafanya ?

Labda tuanzie hapo...
 
Nini Job description ya Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa na Je hio inahitaji degree kuweza kufanya hayo anayotakiwa kuyafanya ?

Labda tuanzie hapo...
Binafsi naamini kwa msomi watanzania hakuna ambaye hajuhi job description ya wenyeviti ila mimi naona wasomi wengi hawataki kwakua haina maslahi makubwa au hakuna maslahi kabisa.
Mfano wangekuwa wanaposho kubwa, au mshahara leo tungeona foleni za watu kugombea.
Nimeshuhudia watu wanapelekewa fomu wanakataa
 
Hatukutakiwa tuwe na Mwenyekiti wa serikali za mitaa, tulitakiwa tuwe na Sheriff.
 
Kuna uzi humu niliweka kuwa viongozi wa juu wa CCM ni akili kubwa,ila huku chini ni vilaza na wajinga
 
Binafsi naamini kwa msomi watanzania hakuna ambaye hajuhi job description ya wenyeviti ila mimi naona wasomi wengi hawataki kwakua haina maslahi makubwa au hakuna maslahi kabisa.
Mfano wangekuwa wanaposho kubwa, au mshahara leo tungeona foleni za watu kugombea.
Nimeshuhudia watu wanapelekewa fomu wanakataa
In short kwangu mimi neno Usomi / Wasomi inaweza kuwa disqualification Kwangu mimi Mwenyekiti wa Mtaa ni Mtu wa Watu aliyepo pale kutekeleza shida mbalimbali za watu (always available); kwahio kama ni wasomi hao hao wanaoliuza Taifa letu... I had rather have anyone ambaye yupo pale kwa ajili ya watu no matter idadi ya Vyeti alivyonavyo kapuni
 
In short kwangu mimi neno Usomi / Wasomi inaweza kuwa disqualification Kwangu mimi Mwenyekiti wa Mti ni Mtu wa Watu aliyepo pale kutekeleza shida mbalimbali za watu (always available); kwahio kama ni wasomi hao hao wanaoliuza Taifa letu Had rather have anyone ambaye yupo pale kwa ajili ya watu no matter idadi ya Vyeti alivyonavyo kapuni
Hakika upo sahihi
 
usiandike kitu bila tafiti,katika vijiji karibu vyote nimetembea nchini ,CHADEMA inawagombea na nyumba 10 ,uchumi wako vizuri na elimu Yao haijaishia kuweza kusoma na kuandika tu
Sijakataa, ila umeelewa nilichosema?? Ndymana nimesema tusilete siasa
Ipo hivi usemalo ni sahihi kuna mikoa ambayo ina uchumi wa juu wagombea wengi ni wapo vizuri kiuchumi ata kielimu.
Mfano Arusha, DSM, Kilimanjaro, Mbeya.
Lakini ukirudi kwa asilimia kubwa wengi wao shule hamna
 
Ni kweli kabisa! Jamii nyingi mitaani ni masikini na wajingawajinga fulani hivi kiasi kwamba kwa mjinga mwenzao ni rahisi kuendana nao!
 
Back
Top Bottom