Fisherscom
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 1,763
- 766
Hilo ndilo kundi linalo ongoza kwa kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Wanaume wengi wanadhani kila mvaa pete ya ndoa ni mke wa mtu na kujipa moyo kwamba yuko ndani ya ndoa na hatokuwa na virusi/ukimwi. Pia wengine wanakimbilia huko kwa kutegemea unafuu wa kumgharamia kwamba kila kitu anapewa na mumewe. Baadhi ya kina dada wanaojiuza wamebuni huo mtindo baada ya kuona soko kubwa limemilikiwa na wake za watu. Upeo wangu ni huo sijui wadau wengine wanalionaje hili suala.
wengine wanajivalisha ili kuwaringishia mashoga zao kuwa na wao wameingejiwa,ila ni upuuzi usio na kifani,ila zinasaidia,kuna kipindi nilikuwa navaa pete inayofanana na ya uchumba sio siri ilinipunguzia kero,japo kuna vichwa ngumu wanaojifanya hawaioni!
Wengine wanavaa kama part ya accessory tu, no meaning. Wengine ni identity crisis, na wale walioahidiwa ndoa hewa, na wachumba walioenda kusoma ulaya.
Advise be a person of your own identity, be single and be proud of that! Kama Mungu hajasema ndio hauwezi hata siku moja kulazimisha.
You will buy the most expensive ring but its urself u are fooling....
Dhambi kubwa sana kudanganya status 'feki'
Eti uonekane umeolewa kumbe siyo,
Utapewa mwanaume ambaye ni mtata hivyohivyo,
Kipimo upimacho ndicho utakachopimiwa na ufalme wa Mbinguni sababu umedanganya hapo,
Ukitangaza kupitia hizi mipete ya uchumba/ndoa wakati wala hata huko hujafika utapewa yule ambaye tayari ameshaoa mke/wake kadhaa au mwenye mikosi kadhaa.
Acheni hizo ishi kama mlivyo sawasawa na macho ya Mungu,kama hujachumbiwa ishi kama vile hujachumbiwa,kama hujaolewa ishi kama hujaolewa sawasawa na Mungu alivyokuweka wewe katika maisha yako!
Kazi njema!
Habari ndio hiyo.
Zaidi, hata wasichana siku hizi hawataki kuolewa. Wanawinda wanaume walioa, wawajengee nyumba na kuwanunulia magari. Wanapendelea wanaume waliooa kwa sababu wanajiheshimu, wako busy na familia. Hii inawafanya wasichana kupata muda free kujirusha na kufanya mambo ya maendeleo independently kuliko kuolewa ambapo ina kuwa kana unalea JIPU LA KWAPA.
Ya nini kuolewa?
i like this yani jino kwa jino
I can't agree more!