Leo kuna swali liliulizwa na Pareso Mbunge maalum toka CHADEMA akiuliza ni "Kwa nini wakandarasi wa kigeni wanalipwa riba kwa kucheleweshewa malipo yao tofauti na wakandarasi wazawa ambao hawalipwi riba pindi wakicheleweshewa malipo yao"?.
Mjibu swali alikuwa Waziri wa Fedha ambaye alijibu tofauti kabisa na swali lililoulizwa. Ni masikitiko makubwa kwa wakandarasi wa ndani wanaodai malipo yao hadi miaka miwili ili hali walichukua mikopo Benki na hawajalipwa hata senti moja kwa kazi waliyokamilisha kwa ukamilifu na ubora kabisa.
Leo hii Waziri anatoa majibu mepesi na yasiyo na tija. Je Serikali imeishiwa fedha?. Je mbona wakati wa Hayati Magufuli walikuwa wanalipwa kwa wakati?.
Je Serikali ina mkakati gani ili wakandarasi waweze kulipwa pamoja na riba?. Je Serikali haiujui kuwa kutolipwa wakandarasi kumepunguza mzunguko wa fedha mitaani?. Tunaomba Wakandarasi wazawa walipwe madai yao ikiwemo riba.