Kwanini wakoloni wetu wanatuomba radhi sasa?

Kwanini wakoloni wetu wanatuomba radhi sasa?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tangu wakoloni waondoke Tanzania na Kenya ni miaka zaidi ya 60 na kwa ujerumani ni miaka zaidi 100 Sasa.

Kwanini Rais wa ujerumani na mfalme Charles warudi Leo kutuomba msahama juu wa Yale mabaya waliyotutendea? kwanini sasaa?

Tusibweteke na msahama huu, bali tuangalie kile ambacho hakikusemwa hadharani walichokuja nacho. Mkoloni kuomba msahama ni athabu kubwa sana inayomdhalilisha, tuhangaike na kwanini wanaomba msamaha Leo na Sasa.

Wanataka nini kwetu? Wanataka kufanya nini kwetu? Wanasukumwa na nini kuomba msamaha Sasa?

Je, ni msamaha TU au wanatulipa watu na rasilimali zetu walizosombea kwao?

Tuwaze nje ya box ili tuwe tofauti na akina Mangungo wa Msovero.
 
Hii misamaha wanayoombaga kwangu ni unafiki mtupu, na ukiwabana zaidi watakuambia sisi tunawaomba msamaha kwa madhila waliyoyafanya babu wa babu zetu kwenu.

Ukirudi upande wa pili mpaka choo anachotumia huyo mfalme kimenakishiwa na madini/vitu walivoiba kwetu, ningemuona si mnafiki kama angesema sitaki tena kutumia au kukaa kwenye kasri lililonakshiwa kwa vitu vya wizi, bomoeni na vitu hvo virudi vilikotolewa, sitaki kuishi na vitu najisi mimi, na naamuru kuanzia leo kila mwaka nchi zote zilizotawaliwa kimabavu na nchi yangu watakuwa wanalipwa fidia ya dollar kadhaa, tofauti na hapo arudishe unafiki uk.
 
Wanataka kurudi kama hao waarabu walivyorudi
 
Nafsi zinawasuta ngoja waje tutawajua wote maana niliona kule uholanzi nao wanaomba msamaha ,ila tulisoma Dutch settlement tu ,kumbe walifanya na utumwa pia.
 
Si kweli. Hii ni danganya toto na wamekuwa wakifanya hivyo tangu zamani. Ili kuonesha kwamba wanajutia walichokifanya hawana budi kulipa na kutoa fidia kwa wahanga wa matukio waliyoyafanya. Hadi leo baadhi ya vichwa vya machifu walivyochukua kupeleka makwao havijarejeshwa nchini. Bado wamekaa na Mjusi wetu toka Tendaguru na wanapata pesa kupitia huyu Mjusi bila hata kutoa kitu kidogo kwetu. Waliwaua watu na machifu wao na kuwanyang'anya ardhi yao pasi na kutoa fidia yeyote. Yapo mengi tu waliyowafanyia mababu zetu na kuomba radhi kwa maneno tu hakuyaondoi machungu waliyonayo baadhi ya Wananchi. Wafanye hivyo kwa vitendo pia.
 
Tangu wakoloni waondoke Tanzania na Kenya ni miaka zaidi ya 60 na kwa ukerumani ni miaka zaidi 100 Sasa.

Kwanini Rais wa ukerumani na mfalme Charles warudi Leo kutuomba msahama juu wa Yale mabaya waliyotutendea?

Tusibweteke na msahama huu bali tuangalie kile ambacho hakikusemwa hadharani walichokuja nacho. Mkononi kuomba msahama ni athabu kubwa sana inayomdhalilisha, tuhangaike na kwanini wanaomba msamaha Leo na Sasa.

Wanataka nini kwetu? Wanataka kufanya nini kwetu? Wanasukumwa na nini kuomba msamaha Sasa?

Je, ni msamaha TU au wanatulipa watu na rasilimali zetu walizosomba?

Tuwaze nje ya box ili tuwe tofauti na akina Mangungo wa Msovero.
wanapitia mlango wanyuma kuja ku2unyonya tena,,walikuwa wanategemea maliasili nyingi kutoka RUSSIA,kama gesi nanafaka,sasa RUSSIA kakaza,ata mali kutoka YKRAINE kupeleka ulaya,RUSSIA kafunga mlango wa bahari hamna meli kupita,,,zen anaza ishu, ni kwamba mataifa ya afrika taratibu yameanza kujitambua,tumeona huko afrika mangaribi,,,,wafaransa wanafukuzwa nawale madalali wao {serikali za kifisadi]zikipinduliwa,leo hii ufaransa kichwa kinamuuma,jamaa wamekomaa hawatki kutoa uranium,wakati wafaransa wanategemea umeme wa uranium,,,unaona bwana,,,kina ki2 kimejificha ata kwa spika we2 wa bunge kupata kuwa rais wa mabunge duniani!!!!!,[sio kwamba napinga au ninakejeli,hapana,nimefurahi sana kwa bendera yetu kukaa juu,,,,]ila,,,[kwa liosoma cuba wataelewa,,,,,jamaa wanatia grisi vyuma vilegee.....si unaona wagombea karibu wote walitokea afrika chalii yangu????.......jue ata obama alivochaguliwa kuwa rais wa amerika usifikiri alibahatisha,,,ule ulikwa mkakati maasusi ulioandaliwa na C.I.A,MOSSAD na M15...kuhakikisha anaingia m2 mwye damu kutoka afrika ambaye hana asilili ya utumwa{asili ya obama ni kenya sio kama kina 50cent],,,umeona bwana,,alaf kukawa na maniga kti sekta nyeti kama mkuu wa majeshi general POWEL{mweusi kizazi cha utumwa],,waziri wa mambo ya nje{kondoleez rice]...na wengineo,,,lengo lake unajua ni nini?.....kuhakikisha wanapindua serikali ya LIBYA chini ya utawala wa GADAFI,,kwani walikuwa wanhofia sera yake ya kuwa serikali yenye muungano afrika,jeshi moja na sarafu moja,,wakaona eeeh!!!!!.......hatari,,,kwa nini walifanya ivo kuweka weusi tupu kwenye top management ya USA,,,,ni kupunguza kelela za dunia kama kianRUSSIA,CUBA,IRAN na mataifa mengine yasiyopenda unyonyaji,kwamba ingekuwa ni wazungu tupu wapo top pale serikalini USA kelele zingekuwa kwamba wazungu wanataka kuitawala tena AFRIKA,,,na kweli walifanikiwa!!!!!!!!!!!!!!!!!1.......mmeona jombaaaaaaaaaaaaaa!!!
 
Binafsi naona huo msamaha hauna maana yoyote
Wangerudisha dhahabu na madini mengine waliyoiba au basi wafute madeni yetu yote na waje na misaada ya kueleweka ndio waombe msamaha......
Yaani watuibie mali zetu za mabilioni na kutesa watu wetu, halafu waje mikono mitupu kuomba msamaha?
 
Hii misamaha wanayoombaga kwangu ni unafiki mtupu, na ukiwabana zaidi watakuambia sisi tunawaomba msamaha kwa madhila waliyoyafanya babu wa babu zetu kwenu.

Ukirudi upande wa pili mpaka choo anachotumia huyo mfalme kimenakishiwa na madini/vitu walivoiba kwetu, ningemuona si mnafiki kama angesema sitaki tena kutumia au kukaa kwenye kasri lililonakshiwa kwa vitu vya wizi, bomoeni na vitu hvo virudi vilikotolewa, sitaki kuishi na vitu najisi mimi, na naamuru kuanzia leo kila mwaka nchi zote zilizotawaliwa kimabavu na nchi yangu watakuwa wanalipwa fidia ya dollar kadhaa, tofauti na hapo arudishe unafiki uk.
WANGEOMBA MSAMAHA HUKU WANATUKABIDHI RAMANI ZA SEHEMU WALIZOFI CHA MALI ZETU WATUPE NA PASSWORD [emoji360]
 
Si kweli. Hii ni danganya toto na wamekuwa wakifanya hivyo tangu zamani. Ili kuonesha kwamba wanajutia walichokifanya hawana budi kulipa na kutoa fidia kwa wahanga wa matukio waliyoyafanya. Hadi leo baadhi ya vichwa vya machifu walivyochukua kupeleka makwao havijarejeshwa nchini. Bado wamekaa na Mjusi wetu toka Tendaguru na wanapata pesa kupitia huyu Mjusi bila hata kutoa kitu kidogo kwetu. Waliwaua watu na machifu wao na kuwanyang'anya ardhi yao pasi na kutoa fidia yeyote. Yapo mengi tu waliyowafanyia mababu zetu na kuomba radhi kwa maneno tu hakuyaondoi machungu waliyonayo baadhi ya Wananchi. Wafanye hivyo kwa vitendo pia.
Kama ni kulipa wawalipe watanganyika wote, hakuna mtanganyika ambae babu yake hakunyanyaswa, kutwezwa na kuibiwa nguvu na mali zake na wakoloni. Wakoloni waliwaswaga watu wajenge reli, barabara na kulima mashamba yao bila idhini yao, kuna wengine waliporwa ardhi zao na maliasili zao. Kama ni kulipa walipe watu wote.
 
Back
Top Bottom