Kwanini wale watengeneza propaganda, hawamwandami Mrema aachie uongozi wa TLP, badala yake wanamng'ang'ania Mbowe tu?

Kwanini wale watengeneza propaganda, hawamwandami Mrema aachie uongozi wa TLP, badala yake wanamng'ang'ania Mbowe tu?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Baada ya kushuhudia Mwenyekiti wa chama cha siasa cha TLP, Mheshimiwa Mrema akijichukulia "dogodogo" na akifunga ndoa majuzi, ambayo ilileta msisimko mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, nilijiuliza maswali kadhaa, kutokana na hali niliyomwona nayo, ya kushindwa kunyanyuka kwenye kiti na kuweka saini kwenye Cheti cha ndoa, huku mikono ikimtetemeka!

Pamoja na kuonyesha "kuchoka" huko kwa Mzee Mrema, lakini bado ma-propragandists wa Sisiem, hawaoni umuhimu wa kumshinikiza Mzee wetu, ang'atuke kwenye kuiongoza TLP na kuwaachia vijana Ili waongoze.

Kwa kuwa ninavyofahamu Mimi, Mzee Mrema amekigeuza chama cha TLP kama mali yake binafsi na hakuna wa kumng'oa kwenye uenyekiti wa hicho.chama, ambacho amekuwa akikishikilia tokea miaka ile ya mwishoni ya 90, baada ya kutoka kwenye chama cha NCCR Mageuzi.

Hata hivyo nawashuhudia hao ma-propragandists wa Sisiem, wakiendelea "kumkomalia" Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, eti ndiyo ang'atuke kwa kukaa muda mrefu kwenye kiti hicho cha uenyekiti!

Niwaulize hao ma-propandists wa Sisiem, hivi hawaoni namna wenyeviti hao wengine wa vyama vya upinzani, kama vile Augustine Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP, namna walivyovigeuza hivyo vyama, kama mali yao binafsi, badala yake kelele zao "wanazipiga" siku zote kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema?
 
Mwambie Mbowe aendelee kukumbatia CHADEMA kama walivyofanya hao halafu ushuhudie anguko la chadema

Akifanya yeye ni mmiliki wa chadema basi chadema hakitakuwa na tofauti na hivyo vyama ulivyovitolea mfano
 
Kwahiyo Hadi Mbowe "achoke kama Mrema"


Ashindwe hata kusimama ndo watu watakuwa na haki ya kumwambia aachie ngazi?

Seriously?..
 
Kama wewe sio mwanachama wa Chadema huna haki ya kumuambia Mbowe aachie ngazi, kama wewe ni mwanachedema na hupendezwi Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti basi hamia ACT, CCM, UDP n.k

Hata wale ambao hawakupendezwa Bashiru Ally kufanywa Katibu mkuu wao kwa sababu walikuwa hawajui chama chake walikuwa na machaguo hayo au kukaa kimya.
Kwahiyo Hadi Mbowe "achoke kama Mrema"
Ashindwe hata kusimama ndo watu watakuwa na haki ya kumwambia aachie ngazi?
Seriously?..
 
Back
Top Bottom