WALOLA VUNZYA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 7,154
- 7,155
Haiwezi anguka kama Magufuri kudanganywa kote kuiua CHADEMA amejikuta akiuliwa bila ya kutegemea na Mbowe akibaki na CHADEMA yake.Mwambie mbowe aendelee kukumbatia chadema kama walivyofanya hao halafu ushuhudie anguko la chadema
Akifanya yeye ni mmiliki wa chadema basi chadema hakitakuwa na tofauti na hivyo vyama ulivyovitolea mfano
Kwa wajinga wenzio ambao ni familia ya mwendazake.Kuna NGO ambazo nazifahamu na sio vyama vya siasa.
1. Chadema 2. TLP 3. UDP.
Unaongea wewe kama nani vile ndani ya CHADEMA?Kwahiyo Hadi Mbowe "achoke kama Mrema"
Ashindwe hata kusimama ndo watu watakuwa na haki ya kumwambia aachie ngazi?
Seriously?..
Wapo wengi, Lipumba, Mbatia n.kBaada ya kushuhudia Mwenyekiti wa chama cha siasa cha TLP, Mheshimiwa Mrema akijichukulia "dogodogo" na akifunga ndoa majuzi, ambayo ilileta msisimko mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, nilijiuliza maswali kadhaa, kutokana na hali niliyomwona nayo, ya kushindwa kunyanyuka kwenye kiti na kuweka saini kwenye Cheti cha ndoa, huku mikono ikimtetemeka!
Pamoja na kuonyesha "kuchoka" huko kwa Mzee Mrema, lakini bado ma-propragandists wa Sisiem, hawaoni umuhimu wa kumshinikiza Mzee wetu, ang'atuke kwenye kuiongoza TLP na kuwaachia vijana Ili waongoze.
Kwa kuwa ninavyofahamu Mimi, Mzee Mrema amekigeuza chama cha TLP kama mali yake binafsi na hakuna wa kumng'oa kwenye uenyekiti wa hicho.chama, ambacho amekuwa akikishikilia tokea miaka ile ya mwishoni ya 90, baada ya kutoka kwenye chama cha NCCR Mageuzi.
Hata hivyo nawashuhudia hao ma-propragandists wa Sisiem, wakiendelea "kumkomalia" Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, eti ndiyo ang'atuke kwa kukaa muda mrefu kwenye kiti hicho cha uenyekiti!
Niwaulize hao ma-propandists wa Sisiem, hivi hawaoni namna wenyeviti hao wengine wa vyama vya upinzani, kama vile Augustine Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP, namna walivyovigeuza hivyo vyama, kama mali yao binafsi, badala yake kelele zao "wanazipiga" siku zote kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema?
Kumbe?Mrema ni mwanachama mtiifu wa Ccm na chama chake ni tawi la Ccm.
Hata hii issue ya harusi feki kutangazwa sana ilikuwa ni mkakati wa Ccm kuua mapokezi ya Mbowe mtaani.
Wewe hujaona sasa ni Mrema tuu Mbowe katulizwa??
Ccm ni laana.
Na ndiyo sababu wanamuachia Mzee Mrema, awe Mwenyekiti wa Maisha wa chama chake!Umenena vema,hao ma-propandists wa ccm wanaamini kuwa siku Mbowe akiondolewa kwa njia yoyote ile watapata unafuu wa kufanya siasa zao chafu,na kutawala milele.
Mada ifungwe...kapata jibu itakuwaje kwa wale wengine wa kudumu anayemteteaKaachia rasmi
Baada ya kushuhudia Mwenyekiti wa chama cha siasa cha TLP, Mheshimiwa Mrema akijichukulia "dogodogo" na akifunga ndoa majuzi, ambayo ilileta msisimko mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, nilijiuliza maswali kadhaa, kutokana na hali niliyomwona nayo, ya kushindwa kunyanyuka kwenye kiti na kuweka saini kwenye Cheti cha ndoa, huku mikono ikimtetemeka!