Kwanini walimu wa Economics wasifundishe somo la Bussiness study (commerce)?

Kwanini walimu wa Economics wasifundishe somo la Bussiness study (commerce)?

Mmea Jr

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Posts
798
Reaction score
1,871
Okay ,, nimejaribu kufuatilia ajira za walimu zilizotoka hivi karibuni na nimegundua kuna uwitaji mkubwa sana wa walimu wa commerce kwa ajili ya kufundisha kidato cha kwanza hadi cha nne

Ndiyo maana utakuja kuona kwenye ajira hizi mpya waombaji wa nafasi ya kufundisha somo la commerce wao katika usahili wataanza na oral moja kwa moja ukilinganisha na wenzao wa masomo mengine ambao wataanza ni written then watakao faulu wataenda oral interview

Sasa basi kwa muda sana nimekuwa nikiona walimu wa Economics wakitumika sanaaa hasa kwenye shule za secondary (o - level ) kufundisha somo la commerce na wengi wamekuwa wakionekana kurimudu viziri tu .

Ushauri wangu kwa serikari,, mtaala mpya unaonesha kidato sha kwanza wanapaswa kusoma somo la business study ambalo zamani ndiyo tuliliita commerce na walimu hao kiidadi imeonesha hawajitoshelezi kabisa kwa shule zote Tanzania ,, sasa kwanini tusiwatumie walimu wa Economics ambao wanarimudu somo hilo na kiidadi wapo wengi ??

Wasiwasi wangu
Tusije kuwanyima fursa walimu wa Economics muda huu wa mchakato wa ajira lakini baadae walimu hawa wa Economics wakifika vituo vya kazi wakaanza kulazimishwa na wakurugenzi kufundisha somo la business study ( Commerce ) kwa kigezo kuwa mwalimu wa Economics hata commerce anaweza kufundisha ..
 
Nashauri somo la book keeping and commerce yafutwe, iweke somo la business study ambalo ndani yake kutakua na ishu za commerce, finance, book keeping ama accounts. Somo liwe comprehensive kuliko ilivyo sasa.
 
Nashauri somo la book keeping and commerce yafutwe, iweke somo la business study ambalo ndani yake kutakua na ishu za commerce, finance, book keeping ama accounts. Somo liwe comprehensive kuliko ilivyo sasa.
Nyie ndio mlichanganyia watoto physics na chemistry bila shaka ...
 
Back
Top Bottom