Kwanini walinda Mlango (goal keepers) wanavaa jezi tofauti na wenzao?

TANZANNIA

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2015
Posts
1,047
Reaction score
385
Nimejiuliza lakini sijapata jibu,hivi ni kwanini ma kipa eidha wanavaa track suit au jezi zenye rangi tofauti na wachezaji wengine,
 
Nimejiuliza lakini sijapata jibu,hivi ni kwanini ma kipa eidha wanavaa track suit au jezi zenye rangi tofauti na wachezaji wengine,
Sababu ni kurahisha utambuzi wa goalkeeper na wachezaje wengine hususani kipindi inapopigwa corner au free kick.

Goalkeeper ndie anaruhusiwa kutumia mikono tu pale wachezaji wanapokuwa wamekusanyika golini
 
Wanavaa hivyo kwa sababu wao ndio wanaruhusiwa kutumia mikono hivyo refa hawezi kuchanganya maamuzi
 
Umeshasema football hivo mikono hairuhusiwi
Ndio, ni football lakini haimaanishi kuwa mikono hairuhusiwi kabisa kutumika.

Kila mchezaji anaruhusiwa kutumia mikono haijalishi ni goalkeeper au la. Isipokuwa, kuna sheria na mipaka ya matumizi ya mikono (limitations).

Hata goalkeeper amewekewa mipaka ya kutumia mikono kuucheza mpira. Goalkeeper pia anaruhusiwa kwenda kushambulia kama wachezaji wengine lakini haruhusiwi kuucheza mpira kwa mikono akiwa nje ya mipaka yake. Akifanya hivyo kinachofuata ni adhabu kwake na timu yake.

Wachezaji wengine pia tofauti na goalkeeper wanaruhusiwa kutumia mikono lakini kama nilivyosema, kuna sheria na mipaka. Mpira unapotoka nje ya eneo la mchezo, unarushwa kwa mikono kurudi mchezoni. Hakuna kosa hapo isipokuwa kama mpira utarushwa isivyotakiwa.

Hata linapokuja suala la mpira kugusana na mikono mchezoni kuna sheria pia (Hand Ball Rule). Mpira unapochezwa na kugusa mikono wakati wa mchezo si kosa. Kosa ni pale ambapo mikono itatumika kama chanzo cha mgusano huo.
 
Hongera kwa ufafanuzi mzuri,
 
Hata goalkeeper anaruhusiwa kurusha mpira hivyo siyo kweli kuwa haruhusiwi kutumia mikono nje ya eneo lake
 
Umeshasema football hivo mikono hairuhusiwi
Sababu ya kuitwa football sio kwamba mpila unapaswa kuguswa na miguu pekee
(foot,feet) sababu ni kwakua wanaocheza hutumia miguu ku move yani kwa lugha ya wenzetu wanasema "on their feet" na sio wheelchair ,rollers ama namna yoyote ile

Ndio maana America kuna american football lakini inachezwa kwa kukamata mpila kwa mikono na kukimbia nao ,ni kama rugby

Hivyo kutumia mikono kwenye mpila wa miguu tena kwa kipa ni sawa na reasonable
 
Nadhani umejibu vema kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa we jamaa ulitaka tu kutengeneza ubishi. Mchezaji tofauti na kipa haruhusiwi kutumia mkono. Sheria ya kwanza ya mpira wa miguu ni uwepo wa uwanja. Ukiwa uwanjani uruhusiwi kutumia mikono isipokua kipa akiwa ndani ya eneo lake. Kurusha mpira manake unauchukua mpira uliotoka nje, ndio maana hata mchezaji anaurusha kwa mikono akiwa nje ya eneo la kuchezea.
 
Hata goalkeeper anaruhusiwa kurusha mpira hivyo siyo kweli kuwa haruhusiwi kutumia mikono nje ya eneo lake
Hazuiwi kurusha ila haruhusiwi kuucheza kwa mikono mpira unapokuwa mchezoni nje ya eneo lake.
 
Mimi nazungumzia mpira wa miguu (football) kwa ujumla, sijazungumzia uwanja wa mchezo peke yake. Usichanganye kati ya mpira wa miguu na uwanja wa mchezo (field of play).

Mpira wa miguu una sheria 17.

Hiyo sheria ya kwanza haihusu urushwaji wa mpira. Urushwaji wa mpira (throw-in) upo chini ya sheria namba 15 ya mpira wa miguu. Tayari hapo kuna utofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…