Kwanini Wamachinga hawaondolewi 'kiakili' miaka nenda rudi?

Ndo shida lipo hapo vizimba Vingi havina machinga wapo wakubwa au wake zao!mfano machinga complex pale vingi machinga wamekodishwa wamiliki wanakula posho na ni vigogo tu!
 

The boss👊
 
Kabisa mkuu ,hawa wanaojiita wamachinga ni wakwepa kodi tu wala hawana lolote,wanataka miseleleko,wanaona wakiwa sehemu rasmi watakuwa wanatoa sehemu ya mapato kwa serikali ambacho hawataki.

Serikali isirudi nyuma,kwa DSM Makala anasema amefanikiwa kwa 80% ,na ni kweli wengi wametoka na baadhi wamechukua fremu zilizopo karibu na walipokuwa wanafanya biashara kwenye mitaro/service road.

Wamachinga wabadili mindset wafanye biashara kidigital,watafute vijana wa IT wawasaidie kuwa na online shopping.
 
Agiza wamachinga wote wajiandikishe manispaa ..chukua data zao zote..
Wametokea wapi?Mikoa ipi?
Idea ya Magu ya kutoa vitambulisho ilikuwa sahihi ila aliifanya kwa kukurupuka sana na kama njia tu ya kukusanya pesa na siyo kutataua tatizonla machinga. Inaweza kuboreshwa.
Bidhaa wanazouza wananunua wapi?
Maduka yapi?
Kwa kawaida machinga wengi wanauza bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa wenye uwezo wa ku-import container au bidhaa za kina Mo, Bakhresa n.k.

Machinga wanaouza bidhaa za kutengeneza wenyewe ni wachache sana.

Mimi ningeshauri kuwa na wizara au hata idara maalum ya kushughulikia biashara ndogo ndogo.
Mitaji Yao iko kiasi gani?
Machinga wapo wenye mtaji kidogo na wengine hawana kabisa. Ukipewa mzigo kazi yako ni kuuza na kulipa boss jioni baada ya kuchukua chako.
Maeneo wanayouza Yana sifa ipi?
Kwa kawaida machinga, palipo na watu ndipp anapouza bidhaa zake.

Na ndio maana hizinstori za kupewa maeneo ya kufanyia biashara hazitakuja kuwa suluhisho hata siku moja.
Kuna watu hata maduka hawana. Mtu anaingiza mzigo kutoka nje. Halafu anaweka ndani godown. Anatoa tu kuwapa machinga kwa makubaliano.
Na ambae Hana location maalum ya kuuza bidhaa asiuziwe..
Machinga anauza sehemu yenye watu. Hahitaji eneo la kufanyia biashara.
Au zile bidhaa kama makava ya simu na mitumba viwe na leseni yake maalum
Ambayo sehemu ya masharti ni kuwa na eneo rasmi la biashara...
May be. Ila sasa nchi hii itakuwa na leseni nyingi sana
Binafsi naona njia rahisi ya kutatua suala la machinga ni "Kukomaa na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo importers".

Pili ni kufanya tathmini ya maduka ya rejareja. Maana unaweza kukuta mtu ana duka la kawaida tu la ku-display kumbe ndaninya nyumna ana tani 200 za mahindi, mchele na crate 100 za pombe lakini anajifanya machinga.

Tatizo la machinga linaanzia kwenye takwimu. Ndio maana Tanzania kuna watu ambao siyo raia na wanaishi tu.

Ikifahamika nani ni nani na anafanya nini itakuwa rahisi
 
Akishakua na eneo maalum,hawi machinga(marching guy)
 
Best post ever! Hii ni big yes nakubalian na wewe... N kuna mmachinga ananunua bidhaa kwa wamachinga wenzie! Ukichunguz kwenye nguo mitumba utalion hili
 
Sehemu zote ambazo machinga wameondolewa ziwe chini ya uangalizi wa JWTZ Kwa kipindi kisichojulikana.Machinga akijichanganya tu inakula kwake mazima. Hapo Ndio tatzo litaisha.vinginevyo michezo itaendelea
Matumizi ya ovyo ya JWTZ
 
Waliolundika machinga haeawezi kulitatua tatizo hili wamechoka
 

Attachments

  • VID-20211013-WA0008.mp4
    4.2 MB
Sasa hivi soko la Karume limeungua moto. Siku wakiruhusiwa tu kuendelea na biashara hapo soko la Karume, nakupa mwezi mmoja tu litarudi kama lilivyokuwa awali.

Na hapo ndio utajua wale unaodhani ni machinga wengine wana mitaji mpaka ya 500M.
 
Kama wao wenyewe hawana akili kwa kulaghaiwa na wana siasa ,lazima uwaonde kwa kutumia jeki Yani 7
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…