Tetesi: Kwanini wanafunzi waliosoma BCom kutoka UDBS hawaitwi katika usaili kutoka tume ya ajira.

Tetesi: Kwanini wanafunzi waliosoma BCom kutoka UDBS hawaitwi katika usaili kutoka tume ya ajira.

mbishi sana

Senior Member
Joined
May 10, 2013
Posts
102
Reaction score
74
Habari wanajamvi!

Mie ni mhimtimu wa shahada katika fani ya biashara (Bcom) kutoka chuo kikuu cha dar es salaam.

Nimeomba nafasi mbali mbali zaid ya kumi za kazi katika tovuti ya ajira bila mafanikio ya kuitwa katika usaili hata mmoja. Nikaona si vibaya kwenda kuuliza labda kuna kitu nakosea.

Majibu niliyoyapata kutoka kwa wafanyakazi wa tume ya ajira ni kuwa sina vigezo vya elimu. Kikubwa waajiri wanahitaj watu wanaosoma shahada ya business administration na sie wa chuo kikuu cha dar es salaam tunasoma shahada ya biashara ya (Bcom).

Na hiyo ndio sababu ya msingi kutoitwa katika usaili wa taasisi hii kongwe ya serikali.

Labda kuwaomba tu wanaotoa matangazo ya ajira hasa katika taasisi za serikal kutotutenga wahitimu wa chuo kikuu cha dar es salaam katika matangazo yao ya kazi. Angalau katika uhitaj wa kazi waweke BA na Bcom ili tukapambane sote katika hizo sahili za kazi.

Naomba kuwakilisha.
 
MMh huo utafiti umeufanya kuanzia lini? ina maana wewe huwa unajua kila anayeitwa au kutoitwa? Si lazima uitwe lazima utambue kuwa uko kwenye ulimwengu wa ushindani na kuna wenzako huwa wanakuzidi vigezo....vuta subra na rekebisha unapo fikiri unakosea.....
 
GPA, walimu wenu wanawakomoa sana, Mmmh wanawafelisha kutaka sifa kumbe wanawaumiza, Nasema GPA zenu ndogo mnaumizwa na walimu wenu

Soma University of Mpitimbi au University of Mwakaleli huko GPA ni kubwa just a joxk
 
Ulishaambiwa ujiajiri wewe bado unatafuta ajira tu tu soli za viatu zitaisha hizo.
 
udsm umekomaa una lower second... wenzetu wanapiga denge anaingia cbe anapiga first class.. ajira mnaomba wote... anapata yeye kwa kigezo cha gpa
 
udsm umekomaa una lower second... wenzetu wanapiga denge anaingia cbe anapiga first class.. ajira mnaomba wote... anapata yeye kwa kigezo cha gpa
Watoto wa cbe wazuri sana kwenye kazi,sijui kwa nini aisee!!?
 
bcom wengi tu wanaitwa kama wewe huitwi ujuepia kuna wengi hawaitwi kwa vigezo vilivyowekwa na tume.
 
Kuna kitu kibaitwa muundo wa utumishi (kama sijakosea) uliandaliwa zamani kwahiyo kuna program yingi sana hazijatajwa kwenye huo muundo hivyo inakuwa ngumu sana kupata kazi siku hizi za awamu ya tano kama program yako haijatajwa kwenye muundo, kuna haja ya wahusika kupitia upya muundo wa utumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom