Mfumo wa elimu Tanzania sijui itakua lini, serikali inashindwa nini kusomesha bure? Asilimia kubwa ya wanafunzi wanaofaulu vijijini wengi wanashindwa kusoma kutokana na wazazi wao kuwa na maisha ya chini. Mwanafunzi anaumiza kichwa kusoma matokeo yake anafanya mtihani na kufaulu lakini anashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa ada. Wadau tujadili kwa pamoja, lini mtoto wa masikini kafika chuo kikuu? Labda wapo lakini watakuwa wamepitia mapito na mahangaiko mengi. Mimi naona bora mfumo wa elimu ibadilishe.