Kwanini wanafunzi wengi wa TZ wanakuwa wachovu katika masomo ya software engineering?

Kwanini wanafunzi wengi wa TZ wanakuwa wachovu katika masomo ya software engineering?

ogm12000

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
304
Reaction score
86
Mimekuwa najiuliza kwa nini wanafunzi wengi wa kitanzania ni wachovu ktk masomo ya software engineering? Je ni waalimu hakuna? au inakuwaje?
Hali hii inajitokeza hasa wanapokwenda nje kufanya master or Phd wengi wanaonyesha uwezo mdogo ktk software courses. Ninayo mifano mingi ya wanafunzi wa kitanzania na kiafrika kwa ujumla hasa wanageria wanakua wachovu sana ktk engineering courses. Wadau tusaidiane ningependa kufahamu tatizo ni nini ktk vyuo vyetu vya kitanzania

Regards
 
.. kwa nini wanafunzi wengi wa kitanzania ni wachovu ktk masomo ya software engineering?
... wanakua wachovu sana ktk engineering courses.
Kuwa specific watu wachambue, unazungumzia software engineering au engineering yote?
... Ninayo mifano mingi ya wanafunzi wa kitanzania
Weka statistics humu, inawezekana hao unaowajua ni nduguzo/watu wa karibu nawe na maybe ni wachache, weka zote au walau sample ya maana ili tuone percentage ya walio wachovu katika scholars wote
 
Mimekuwa najiuliza kwa nini wanafunzi wengi wa kitanzania ni wachovu ktk masomo ya software engineering? Je ni waalimu hakuna? au inakuwaje?
Hali hii inajitokeza hasa wanapokwenda nje kufanya master or Phd wengi wanaonyesha uwezo mdogo ktk software courses. Ninayo mifano mingi ya wanafunzi wa kitanzania na kiafrika kwa ujumla hasa wanageria wanakua wachovu sana ktk engineering courses. Wadau tusaidiane ningependa kufahamu tatizo ni nini ktk vyuo vyetu vya kitanzania

Regards

Unazungumzia Watanzania au Wanaija? Mbona Nimesoma na Watu Kibao pale FOE na ni Watade tu katika hizo Nyanja? Mambo ya OOSE wanagonga sana tu
 
Acheni kumzungusha jamaa bwana. Anachosema kina ukweli bwana.
Elimu ya chuo pale mkuu ya kudesa tu kwa asilimia kubwa. M2 yuko radhi apasue pepa ili awe na GPA ya kutosha tu.
In short wa2 wanakrem sana. Tena wanasoma zile engo ambazo pepa ndo itatokea humohumo.
Ila nakuibia tu kwamba wapo wa2 ambao wako sirias ktk anga ulizotaja. Kuna wanaosoma na wakitaka kuelewa zaidi na wanakua fiti balaa. Bahati mbaya hujakutana na watade hao wachache.
Walimu wabongo nao wanachangia kuwadumaza wanafunzi. Ufundishaji wao wa kubabaisha sana, wako zaidi too academic kuliko ku-deliva vi2 ambavyo vinaendana na wakati na ni chalenj ktk dunia ya sasa.
Naklik Reply...
 
Kuweza kubobea katika katika fani yeyote ya u-engineer iwe electrical, mechnical, civil ........etc etc ni lazima uwe na msingi mzuri wa somo la HISABATI tangu elimu ya mwanzo. Kwa mjibu wa matokeo ya tangu mitihani ya darasa la saba, kidato cha nne na cha sita wanafunzi wengi wanaogopa HISABATI na hivyo wana feli mitihani yake. Sasa hapo huoni uwezekano wa kuwa na wanafunzi wengi(sio wote) wa fani mbalimbali za engineer walio wachovu???
 
Acheni kumzungusha jamaa bwana. Anachosema kina ukweli bwana. Elimu ya chuo pale mkuu ya kudesa tu kwa asilimia kubwa.

FACTS and FIGURES PLEASE

M2 yuko radhi apasue pepa ili awe na GPA ya kutosha tu. In short wa2 wanakrem sana.

Nonsense

Tena wanasoma zile engo ambazo pepa ndo itatokea humohumo.

Wanaona mtihani kabla au wanatunga na walimu?

Ila nakuibia tu kwamba wapo wa2 ambao wako sirias ktk anga ulizotaja. Kuna wanaosoma na wakitaka kuelewa zaidi na wanakua fiti balaa.

Contradicting your nonsenses above

Walimu wabongo nao wanachangia kuwadumaza wanafunzi. Ufundishaji wao wa kubabaisha sana, wako zaidi too academic kuliko ku-deliva vi2 ambavyo vinaendana na wakati na ni chalenj ktk dunia ya sasa.

Contradicting your nonsenses above
 
Unazungumzia Watanzania au Wanaija? Mbona Nimesoma na Watu Kibao pale FOE na ni Watade tu katika hizo Nyanja? Mambo ya OOSE wanagonga sana tu
mkuu OOSE ndio nini??,
hatuiti OOSE, bali ni OOPS (Object Oriented Programming'S), yani mambo ya kutumia objects, classes, methods, inheritance, Abstraction, Polymorphism, Event Handling and Encapsulation.
mambo ya java, .net etc usipime mkuu waTZ tuko dipu balaa sema tunabaniwa hatuwezeshwi wewee, wadosi ndio wanakalia resources zetu zote.
 
Kuwa specific watu wachambue, unazungumzia software engineering au engineering yote?

Weka statistics humu, inawezekana hao unaowajua ni nduguzo/watu wa karibu nawe na maybe ni wachache, weka zote au walau sample ya maana ili tuone percentage ya walio wachovu katika scholars wote

Ninazungumzia course ambazo zina software (programming) kama vile computer engineering, computer science, electronics and control engineering.
Bongo hizi course zinafundishwa lakini ktk programming zinafundishwa ktk kiwango cha chini. Watu wakija kufanya masters utakuta hawana knowledge ya basic things.
Lengo langu nikutaka kujua source ya matatizo haya nini? Na vile vile sijasema kwamba ni wote bali nimesema walio wengi.
Kuna mtu alikuwa point 3 ya mzumbe form six na kupata scholarship amemaliza Bsc ya electronics na gpa kali 3.5/4 lakini matokeo yake ya course zenye programming language sio mazuri kulingalisha na course zingine yani amestruggle kuzifaulu compared na course nyingine. Huo ni mfano wako wengi sana siwezi kuwataja wote. Statistics ktk suala hilo ni hakuna.
Ninaowafahamu mimi ni watu wa karibu ofcourse na wengi wao ni wenye division one kali form six. Nadhani unajua kwenye miaka ya 2000 ulikuwa huwezi kuingia dept hizi pale udsm kama huna one ya point tano kushuka. Course za electrical engineering, civil na mechanical hazina wasiwasi sana wabongo wanazimudu vizuri. Inapokuja issue ya programming acha na program kama java, Asp.net, sisco na zinginezo nyingi watu wanazimudu. In short wabongo course au software za networking hawana matatizo nazo ila programming kama high level language c, c++,assembly, pic programming, labview,dspace, microprocessors na matlab.

In short mimi sio mtu anaeongea bila kuwa na knowledge ya ninavyo ongelea.
ni graduate wa Bsc ya electrical and Electronics dept na nina Msc ya Systems and Control ni
nimefanya programming nyingi tu na watu wa mataifa mbalimbali na watu wa africa wameonyesha uwezo mdogo ktk masuala ya programming.

Watu wengine wa karibu yangu wamefanya course hizi pale mlimani na ata hapa. Wengi wanalalamika kuhusu programming inasumbua.

NB: Usiongee ili kufurahisha genge kuna ki section cha udaku/utani ambacho kinafaaa kwa mambo hayo..

Regards
 
Swali liko too general

Nimeliweka swali kuwa too general kwa kuwa mifano ya watu ninaowafahamu ni jamaa zangu na marafiki zangu wa karibu na nisingependa kuwatolea mifano humu ndani.

In short kama kuna mtu amefanya course yenye programming (software) anaweza kunielewa kwa urahisi zaidi nini nilichouliza. Kwa kifupi mifano niliyo nayo ni marafiki zangu zaidi ya watano ambao ni walipata division 1 ya point 3 na 5 pale mzumbe miaka ya 2000. Walipata scholarship na wamefaulu vizuri tu ktk Bsc degree zao za electronics na computer engineering lkn wamelalamika kuwa masomo yenye programming language kama vile microprocessor (8086 family) kwa watu wa computer engineering, 8051 family kwa watu wa electronics, pic16fxx, pic18fxx, c,c++,matlab,dspace na zinginezo nyingi zinasumbua.

Mifano iko mingi na ndio maana nikataka kujua source ni nini?

Regards
 
ninazungumzia course ambazo zina software (programming) kama vile computer engineering, computer science, electronics and control engineering.
Bongo hizi course zinafundishwa lakini ktk programming zinafundishwa ktk kiwango cha chini. Watu wakija kufanya masters utakuta hawana knowledge ya basic things.
Lengo langu nikutaka kujua source ya matatizo haya nini? Na vile vile sijasema kwamba ni wote bali nimesema walio wengi.
Kuna mtu alikuwa point 3 ya mzumbe form six na kupata scholarship amemaliza bsc ya electronics na gpa kali 3.5/4 lakini matokeo yake ya course zenye programming language sio mazuri kulingalisha na course zingine yani amestruggle kuzifaulu compared na course nyingine. Huo ni mfano wako wengi sana siwezi kuwataja wote. Statistics ktk suala hilo ni hakuna.
Ninaowafahamu mimi ni watu wa karibu ofcourse na wengi wao ni wenye division one kali form six. Nadhani unajua kwenye miaka ya 2000 ulikuwa huwezi kuingia dept hizi pale udsm kama huna one ya point tano kushuka. Course za electrical engineering, civil na mechanical hazina wasiwasi sana wabongo wanazimudu vizuri. Inapokuja issue ya programming acha na program kama java, asp.net, sisco na zinginezo nyingi watu wanazimudu. In short wabongo course au software za networking hawana matatizo nazo ila programming kama high level language c, c++,assembly, pic programming, labview,dspace, microprocessors na matlab.

In short mimi sio mtu anaeongea bila kuwa na knowledge ya ninavyo ongelea.
Ni graduate wa bsc ya electrical and electronics dept na nina msc ya systems and control ni
nimefanya programming nyingi tu na watu wa mataifa mbalimbali na watu wa africa wameonyesha uwezo mdogo ktk masuala ya programming.

Watu wengine wa karibu yangu wamefanya course hizi pale mlimani na ata hapa. Wengi wanalalamika kuhusu programming inasumbua.

Nb: Usiongee ili kufurahisha genge kuna ki section cha udaku/utani ambacho kinafaaa kwa mambo hayo..

Regards
unachoongea ni kweli na huyo mtu anayekuambia stats n data anataka kuleta ubishi.

Mimi ninaona ni maswala ya facilities na walimu.
1. Kozi nyingi za eng zinahitaji computer kwa ajili ya programming. Uni nyingi za ngambo (uk) ukianza first year unapewa laptop ambayo imekuwa loaded na software mbalimbali zinazohitajika. Hii inakusaidia kufanya mazoezi ya mara kwa mara
2. Walimu time wanayowapa wanafunzi ni kidogo sana, wakati ngambo unaweza ukaenda kwa mwalimu mara kwa mara. Pia walimu wa ngambo wanafundisha vitu latest na wanajitahidi kwenda na wakati all the time
 
Kaka naomba uwe makini sana unapotoa hoja.
1. Ulianza na Kwanini wanafunzi wengi wa TZ wanakuwa wachovu katika masomo ya software engineering?

2. Kwanini nilikujibu hivyo:
Naomba ukubaliane na mimi kuwa Software Engineering siyo Programming.
Baadaya hapo ulikuwa specific na kupoint out kuwa issue ni programming? Yes I agree, nina majibu mengi mazuri kwanini hili ni tatizo. Baadhi ya majibu haya mjumbe aliyetangulia amekujibu vizuri tu.
 
Mie mbona nawaona wabongo wengi tu wanapasua hiyo anga ya softii kiulaini tu...pengine labda hilo eneo lako mkuu....
 
Kaka naomba uwe makini sana unapotoa hoja.
1. Ulianza na Kwanini wanafunzi wengi wa TZ wanakuwa wachovu katika masomo ya software engineering?

2. Kwanini nilikujibu hivyo:
Naomba ukubaliane na mimi kuwa Software Engineering siyo Programming.
Baadaya hapo ulikuwa specific na kupoint out kuwa issue ni programming? Yes I agree, nina majibu mengi mazuri kwanini hili ni tatizo. Baadhi ya majibu haya mjumbe aliyetangulia amekujibu vizuri tu.

Thanks kwa comment yako nadhani title ilikuwa haiko very clear lakini nashukuru kuna baadhi ya wadau wameelewa nilichokuwa namaanisha. Nilikuwa nimekusudia zaidi ktk masomo programming. Lakini kama mdau (vitendo) alivyotoa maelezo hakuna tofauti kubwa kati ya programmers na software engineers maana wote wanadevelop programs in different ways.

Regards
 
Mleta mada nakuunga mkono kwa 99.5%.. Ila nakupinga kwenye swala la kusema kuwa hao wanaopata pt3 ilitakiwa wa-perform vizuri kwenye software kisa walifanya vizuri form 6..

Ukweli ni kwamba, Most of government secondary schools are exams oriented and not proffessional oriented.. Mi nimepata kusoma kwenye shule wanazoziita kubwa hapa Tanzania, tena huwa nashangaa wana diriki kuziita special shool(Upuuzi).. Nilikuwa na malengo mazuri sana ya kujijenga ktk elimu kwa vitendo.. Lakini kinachotokea ni upuuzi.. Nimepata kusoma Moshi tech (Electrical installation), yaani shule hii kwa kipindi chetu ilikuwa zero kabisa kwa ku-insist masomo kwa vitendo. Wengi wa watu pale wanatoka empty ktk nyanja za ufundi, the same na shule nyingine za special ni ujinga mtupu unaofanyika pale..

Yaani walimu wanajivunia kushika nafasi fulani kitaifa au kimkoa, bila kuangalia kuwa wanafunzi wao ni wazuri kwa kiwango gani.

Mfumo wa Elimu wa Tanzania ni wa Kijinga na hautatufikisha popote maana siasa imetawala elimu na badala ya elimu kuitawala siasa.

Kuhusu knowledge ktk Computer.. Kuna watoto wa maskini ambao ni wana akili sana. Mtu anafika mpaka form 6 hajui hata Computer inawashwa vp.. Kwa hiyo anapofika chuo kkuu kusoma Computer sc lazima kwanza aanze kujijenga kwa kuijua Computer yenyewe kwanza nini, ili ndo aweze kuiweka vizuri akili yake ktk Computer sc..

Mi naishauri serikali iwekeze kwenye IT, kwa kuwawekea mazingira mazuri wanafunzi wanaofanya vizuri kuanzia O'level na kuendelea..

Mfumo wa elimu wa Tanzania ni moja ya mifumo mibaya kabisa kwa sababu unaendeshwa na siasa na badala ya Elimu kuiendesha siasa..[/SIZE][/SIZE][/B][/B][/B][/SIZE][/COLOR]
 
Back
Top Bottom