.. kwa nini wanafunzi wengi wa kitanzania ni wachovu ktk masomo ya software engineering?
Kuwa specific watu wachambue, unazungumzia software engineering au engineering yote?... wanakua wachovu sana ktk engineering courses.
Weka statistics humu, inawezekana hao unaowajua ni nduguzo/watu wa karibu nawe na maybe ni wachache, weka zote au walau sample ya maana ili tuone percentage ya walio wachovu katika scholars wote... Ninayo mifano mingi ya wanafunzi wa kitanzania
Mimekuwa najiuliza kwa nini wanafunzi wengi wa kitanzania ni wachovu ktk masomo ya software engineering? Je ni waalimu hakuna? au inakuwaje?
Hali hii inajitokeza hasa wanapokwenda nje kufanya master or Phd wengi wanaonyesha uwezo mdogo ktk software courses. Ninayo mifano mingi ya wanafunzi wa kitanzania na kiafrika kwa ujumla hasa wanageria wanakua wachovu sana ktk engineering courses. Wadau tusaidiane ningependa kufahamu tatizo ni nini ktk vyuo vyetu vya kitanzania
Regards
Acheni kumzungusha jamaa bwana. Anachosema kina ukweli bwana. Elimu ya chuo pale mkuu ya kudesa tu kwa asilimia kubwa.
M2 yuko radhi apasue pepa ili awe na GPA ya kutosha tu. In short wa2 wanakrem sana.
Tena wanasoma zile engo ambazo pepa ndo itatokea humohumo.
Ila nakuibia tu kwamba wapo wa2 ambao wako sirias ktk anga ulizotaja. Kuna wanaosoma na wakitaka kuelewa zaidi na wanakua fiti balaa.
Walimu wabongo nao wanachangia kuwadumaza wanafunzi. Ufundishaji wao wa kubabaisha sana, wako zaidi too academic kuliko ku-deliva vi2 ambavyo vinaendana na wakati na ni chalenj ktk dunia ya sasa.
mkuu OOSE ndio nini??,Unazungumzia Watanzania au Wanaija? Mbona Nimesoma na Watu Kibao pale FOE na ni Watade tu katika hizo Nyanja? Mambo ya OOSE wanagonga sana tu
Kuwa specific watu wachambue, unazungumzia software engineering au engineering yote?
Weka statistics humu, inawezekana hao unaowajua ni nduguzo/watu wa karibu nawe na maybe ni wachache, weka zote au walau sample ya maana ili tuone percentage ya walio wachovu katika scholars wote
Swali liko too general
unachoongea ni kweli na huyo mtu anayekuambia stats n data anataka kuleta ubishi.ninazungumzia course ambazo zina software (programming) kama vile computer engineering, computer science, electronics and control engineering.
Bongo hizi course zinafundishwa lakini ktk programming zinafundishwa ktk kiwango cha chini. Watu wakija kufanya masters utakuta hawana knowledge ya basic things.
Lengo langu nikutaka kujua source ya matatizo haya nini? Na vile vile sijasema kwamba ni wote bali nimesema walio wengi.
Kuna mtu alikuwa point 3 ya mzumbe form six na kupata scholarship amemaliza bsc ya electronics na gpa kali 3.5/4 lakini matokeo yake ya course zenye programming language sio mazuri kulingalisha na course zingine yani amestruggle kuzifaulu compared na course nyingine. Huo ni mfano wako wengi sana siwezi kuwataja wote. Statistics ktk suala hilo ni hakuna.
Ninaowafahamu mimi ni watu wa karibu ofcourse na wengi wao ni wenye division one kali form six. Nadhani unajua kwenye miaka ya 2000 ulikuwa huwezi kuingia dept hizi pale udsm kama huna one ya point tano kushuka. Course za electrical engineering, civil na mechanical hazina wasiwasi sana wabongo wanazimudu vizuri. Inapokuja issue ya programming acha na program kama java, asp.net, sisco na zinginezo nyingi watu wanazimudu. In short wabongo course au software za networking hawana matatizo nazo ila programming kama high level language c, c++,assembly, pic programming, labview,dspace, microprocessors na matlab.
In short mimi sio mtu anaeongea bila kuwa na knowledge ya ninavyo ongelea.
Ni graduate wa bsc ya electrical and electronics dept na nina msc ya systems and control ni
nimefanya programming nyingi tu na watu wa mataifa mbalimbali na watu wa africa wameonyesha uwezo mdogo ktk masuala ya programming.
Watu wengine wa karibu yangu wamefanya course hizi pale mlimani na ata hapa. Wengi wanalalamika kuhusu programming inasumbua.
Nb: Usiongee ili kufurahisha genge kuna ki section cha udaku/utani ambacho kinafaaa kwa mambo hayo..
Regards
Nina wasiwasi kama unajua ulichokiandika.
Kaka naomba uwe makini sana unapotoa hoja.
1. Ulianza na Kwanini wanafunzi wengi wa TZ wanakuwa wachovu katika masomo ya software engineering?
2. Kwanini nilikujibu hivyo:
Naomba ukubaliane na mimi kuwa Software Engineering siyo Programming.
Baadaya hapo ulikuwa specific na kupoint out kuwa issue ni programming? Yes I agree, nina majibu mengi mazuri kwanini hili ni tatizo. Baadhi ya majibu haya mjumbe aliyetangulia amekujibu vizuri tu.