Kwanini wanaitana Waheshimiwa? Je, ni lazima kuita hivyo uwapo kwenye mazingira yao?

Kwanini wanaitana Waheshimiwa? Je, ni lazima kuita hivyo uwapo kwenye mazingira yao?

hata mimi

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
1,356
Reaction score
1,442
Viongozi hususani wa kisiasa wamekuwa wakiitwa au wakiitana waheshimiwa sijui sisi wengine tunaonekanaje hata yani!

Utakuta mtu ambae ni mbunge waziri diwani mkuu wa wilaya/mkoa mkurugenzi nk kwenye vikao/mikutano yao neno hilo limetawala hadi kero (kwangu mimi)

Nauliza hivyo maana utasikia mheshimiwa fulani mheshimiwa fulani yaani hata mtu ana title fulani itatajwa lakini neno mheshimiwa lazima lianze, kwanini?
 
Kama taifa nadhani kuna mambo mengi ya msingi kushughulika nayo kuhusu serikali yetu na viongozi wetu. Nadhani kwa hali ya taifa letu kwa sasa nikimaanisha kisiasa, kiuchumi na kijamii ni vyema tukajikita kwenye hoja zenye mantiki kwenye kuliinua taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania.

Ni mtazamo tu.
 
Hayati Mkapa alikataa kuitwa hivyo, aliomba aitwe Ndugu au Bwana Mkapa, nadhani hata Mwalimu Nyerere naye aliomba aitwe Ndugu au Mwl, hawa wanaojiita waheshimiwa ni defensive mechanism ili kujilinda wanapoteleza
 
Viongozi hususani wa kisiasa wamekuwa wakiitwa au wakiitana waheshimiwa sijui sisi wengine tunaonekanaje hata yani!!?

Utakuta mtu ambae ni mbunge waziri diwani mkuu wa wilaya/mkoa mkurugenzi nk kwenye vikao/mikutano yao neno hilo limetawala hadi kero (kwangu mimi)

Nauliza hivyo maana utasikia mheshimiwa fulani mheshimiwa fulani yaani hata mtu ana title fulani itatajwa lakini neno mheshimiwa lazima lianze, kwanini?
Me huwa nawaita weh jamaa
 
Tafuta hela mkuu. Ukiwa na hela mtaani unaitwa mheshimiwa hata kama una butcher la nyama.

Ukiwa na kitambi na hauna hela utatukanwa hadi na bodaboda watasema una minyoo.
 
Back
Top Bottom