OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Mara ya kwanza mbunge wa Gairo alishauri laini zitozwe TSh 200 kila mwezi. Na sasa huyu mwingine ameshauri laini itozwe Tsh 50. Kwanini wanaona ni muhimu kutoza laini za simu? Ni rahisi lakini je kitendo hiki ni halali kwa watanzania ambao wanahangaika kumiliki simu nk. Je hatuoni kuwa zitaongeza mgawanyo wa kidigitali?
Ninachokiona kwa ushauri wa kutoza kodi laini za simu ni kusema tumeshindwa kuona namna sahihi ya kupata kodi kwenye maeneo ambayo yanafedha nyingi na kuja kuwakamua raia kwenye huduma hii muhimu. Mawasiliano ni jambo muhimu na la haki ambalo linatakiwa lipatikane kwa gharama nafuu, haya maneno ya mara kwa mara ya kutaka kutoza kodi yatawanyima watu haki ya kuwasiliana kwa hawa watanzania ambao anakaa mwezi hajaweka salio zaidi ya kubipu tu ili apigiwe.
Kwasasa watu wengi wamekuwa wakishare video ya Magufuli akiwalaumu TRA kuwa wanakosa ubunifu wa kukusanya kodi. Nadhani ni kweli, na tunapoendea kuna uwezekano mkubwa wa watu wasio na fedha kulipa kodi kubwa huku wanaotakiwa kulipa kodi za kuinua nchi wakaachwa wanainjoi maisha yao.
Nitoe wito kwa TRA, Wizara ya fedha nk, hebu itisheni papers halafu muone mawazo makali ya ukusanyaji kodi mtakayoyapata kutoka kwa wadau badala ya kukimbilia kutoza kodi kwenye laini.
Wito wangu kwenu ni kuwa, kwa wakati huu inabidi tuitumie digitali kupata kodi, sio kuitoza kodi digitali.
Nawasilisha
PIA SOMA
- Mbunge Santiel Kirumba: Kila laini ikatwe Tsh. 50 tujenge barabara