Juma Issihaka
New Member
- Sep 25, 2019
- 3
- 3
Unakumbuka, siku moja baada ya ajali ya moto katika soko la kariakoo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliunda kamati ya siku saba kubaini chanzo chake?
Tukio hilo lililotokea Julai 11, mwaka 2021 na kusababisha hasara kwa maelfu ya wafanyabiashara katika Soko hilo kongwe jijini hapa, licha ya kamati kupewa siku hizo ni mwaka sasa haikuwahi kutoa jawabu la swali ililoenda kulifanyia kazi.
Kadhalika, Machi 12, mwaka jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jaffo aliunda kamati kuchunguza athari za maji ya Mto Mara mkoani Mara.
Pamoja na kuhusisha wataalamu kutoka idara mbalimbali za Serikali, lakini majibu iliyokuja nayo yaliushangaza umma, baada ya kudai kinyesi cha wanyama hasa Ng’ombe ni moja ya sababu ya uwepo wa sumu inayoangamiza viumbemaji katika Mto huo.
Kama hiyo haitoshi, mauaji ya Mtwara yaliundiwa kamati ya watu tisa iliyopewa jukumu la kufanya uchunguzi kwa siku 14, lakini hadi leo ni miezi mitano haikuwekwa hadharani nini kilibainika na kamati hiyo.
Vile vile, ajali tano za moto katika vipindi tofauti ndani ya soko la Karume, zote ziliundiwa kamati lakini kumekuwa na kujirudia kwa matukio hayo na tukio la mwisho lilitokea Januari 15, mwaka huu.
Kuundwa kwa tume na kamati mbalimbali hakujaaza leo. Mwaka 1996 Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa aliunda tume dhidi ya rushwa serikalini.
Licha ya kutoka na mapendekezo mazuri, yamebaki kuachwa makabatini.
Hiyo ni mifano michache kati ya mingi ya kamati na tume zilizowahi kuundwa na Serikali kushughulikia mambo mbalimbali nchini, lakini hazikujibu vitendawili vya matukio husika na kusababisha isionekane tija ya kuundwa kwake.
Hatua hiyo, imeondoa imani ya wananchi juu ya tume na kamati hizo na hilo ndilo linalofanya hivi sasa Tume ya Kuangalia na kuboresha mfumo wa taasisi za haki jinai itiliwe mashaka.
Hofu ya wengi si mapendekezo mazuri yanayotokewa, bali ni utekelezwaji wa kinachopendekezwa.
Mashaka kuhusu tume haki jinai
Pamoja na utashi na nia njema ya utekelezwaji wa mapendekezo hayo ambayo aghalabu huelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Mhadhiri Msaidizi wa Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Revocatus Kabobe anasema kuna mashaka ya hilo kufanyika.
Mashaka hayo yanatokana na kile anachoeleza kuwa, baadhi ya mapendekezo ya tume hiyo yanakinzana na mfumo wa utawala wa nchi.
“Baadhi ya mapendekezo yanakinzana na mfumo wa utawala wa nchi kwa mfano lile la kutaka mabadiliko ya utendaji wa Jeshi la Polisi kutoka kutumia nguvu ‘Police Force’ hadi kutoa huduma ‘Police Service’.
“Hii inahitaji kufumua mfumo mzima wa jeshi hilo na hilo ni vigumu kutekelezwa bila kufanya mabadiliko ya Katiba yote,” anasema.
Kabobe anaeleza kunapaswa kuwe na maboresho ya mfumo wote wa sheria zetu unaohusisha Katiba ili kufanikisha kutekeleza baadhi ya mapendekezo.
Hoja ya Kabobe inaungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki Taarifa, John Kitoka anayesema kwa sehemu kubwa mapendekezo yaliyotolewa yanahitaji mabadiliko ya mfumo mzima wa sheria.
Kwa sababu hiyo, anaeleza mapendekezo hayo yanailazimu Serikali kuendeleza na kuharakisha mchakato wa Katiba Mpya ambayo ndiyo sheria mama.
“Mapendekezo mengi hayawezi kutekelezeka bila kubadilisha vifungu vya Katiba, hivyo utekelezwaji wake utahitaji mabadiliko makubwa ya sheria ambayo Katiba ipo ndani yake,” anasema.
Pamoja na hilo, Kitoka anasema baadhi ya mapendekezo hayo yanahitaji mabadiliko ya sheria yatakayoipunguzia dola madaraka.
“Kwa sababu mara nyingi watawala hawapendi sheria ambazo zinawapunguzia mamlaka, nachelea kusema kwamba mapendekezo hayo yatatekelezwa,” anasema.
Tofauti na mitazamo ya Kitoka na Kabobe, kulikuwepo matumaini ya utekelezaji kutoka kwa Mhadhiri wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idd Mandi anayesema tume zinazoundwa kwa ajili ya masuala ya kisheria nyingi utekelezaji hufanyika.
“Kuna ile tume ya Pius Msekwa ilitoa mapendekezo mbalimbali na yalisababisha kutungwa kwa sheria nyingi, pia kuna ile tume ya Mark Bomani, ilipendekeza kuanzishwa kwa Shule ya Sheria na hiyo imeanzishwa.
“Changamoto ya utekelezaji ni kwenye tume zinazoanzishwa kushughulikia masuala ya siasa na huko mimi sijui,” anasema.
Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba, Bob Wangwe anasema anasita kuamini kwamba mapendekezo yaliyotolewa na tume hiyo yatatekelezwa.
“Napata kigugumizi kusadiki kwenye maneno isipokuwa natamani na nitakuwa na amani nikiona kuna utekelezaji, tumekuwa na tume nyingi lakini utekelezaji umekuwa si mzuri au haupo,” anasema Wangwe.
'Hazieleweki'
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga anasema bado haijaeleweka kwamba kamati na tume hizo zinaundwa kuwasahaulisha wananchi au zinalenga kurekebisha changamoto zinazojitokeza.
Mkurugenzi huyo anasema kamati zinazoundwa zinapaswa kujifunza katika majanga yanayotokea ili kutengeneza mbinu za kukabiliana nayo pengine yasitokee tena au kuwe na urahisi wa kuyadhibiti yatakapotokea lakini hilo halijafanikiwa nchini.
“Tulitarajia mapendekezo na matokeo ya kamati hizo yawekwe wazi, kwamba jamani tuligundua hili limesababishwa na jambo hili na kuanzia sasa tunapaswa kutunga sheria kudhibiti hili, kwa mfano,” anasema.
Kwa vitendo hivyo, anasema haki ya kumiliki mali na kuishi inakiukwa.
Tatizo zinavyoundwa
Onesmo Ole Ngurumwa ni Mkurugeni wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), anasema changamoto ya kamati na tume hizo huanzia kwenye uundwaji wake.
"Kinachochangia kamati na tume kukosa tija ni kuanzia kwenye uundwaji wake kwa mfano ile kamati iliyoundwa kuchunguza mauaji Mtwara hadi leo haikuja na jawabu," anasema.
Anapendekeza kuundwa kamati za kudumu za kushughulikia mambo mbalimbali ambazo uundwaji wake uzingatie uhuru, kwa maana watu kutoka kada mbalimbali wahusishwe si serikalini pekee.
Akizungumzia hilo mtaalamu wa udhibiti wa majanga, James Mbatia anasema kutotekelezwa kwa sheria ya udhibiti na kujikinga na majanga ya mwaka 2015 ndiyo sababu ya yanayoendelea kutokea.
Anasema mwaka 2015 akiwa bungeni alitumia utaalamu wake kwa kushirikiana na wengine kufanya utafiti ili kutengeneza sheria hiyo, ambayo hadi sasa haitekelezwi.
“Katika sheria ile tulipendekeza kuundwa kwa wakala au taasisi ya udhibiti wa majanga, lakini hadi leo haijaundwa. Serikali inasema haina fedha za kufanya hivyo,” anasema.
Anasema ili kupata utatuzi wa haraka wa majanga yanayotokea na kuundiwa tume ambazo hazionyeshi tija ya kuundwa kwake, unahitajika utekelezwaji wa sheria hiyo.
Kulingana na Ibara ya 3 ya sheria hiyo, Wakala wa Udhibiti wa Majanga, utawajibika kukinga majanga au matishio, kupunguza ukali au msururu wa maafa, kutengeneza mbinu thabiti za kujiandaa na maafa, kutengeneza njia bora ya kuokoa baada ya majanga na njia ya kuitikia maafa.

Upvote
0