Gbollin,
Kabla ya "Beijing" kuwa sera rasmi ya dunia...
kama huijui hii "Beijing" mtafute mama G. Mongela atakufahamisha vizuri.
Wanaume katika jamii nyingi, nafikiri sio kwa baadhi ya makundi ya wahindi, hawa familia ya mwanamke ndio inalipa mahari, ndio walikuwa wawindaji, watafutaji na wanawake walimilikiwa na kufanya kazi za nyumbani...
Kwa hiyo hizo za mahari zilianza hivyo,kwa sababu wanawake walikuwa hawana wanachomiliki, bali wao walimilikiwa.
Si unajua tena jamii zinavyopenda kuendeleza mila na desturi..kurithishana desturi hata kama ni mbovu na kuziendeleza?
kwa jamii nyengine, mahari ni ishara ya mahaba, mapenzi,, mwanamme huwa anaungama mapenzi,upendo wake kwa mke mtarajiwa na familia yake. ni zawadi ya kuunga udugu. kama kiwango ni wastani basi ni ishara tu, zawadi kwa mwanamke na sio bei ya manunuzi ya mke.
kwa hiyi mila na desturi ya mahari itaendela kwa muda mrefu tu, hadi pale watu watakaposhindwa kulipa mahari, wataanza kuchakachua...watu wa mijini wanaanza kuiga mila za ulaya,,mahari less ndoa! Ndoa za mahakamani na kwa mkuu wa mkoa au wilaya.