Kwanini wanawake hamna huruma?

Hehehe nilijua mtafikia hapa.

Bando la kwake.
Device ya kwake
Akili ya kwake
Maoni yake.

Sisi haswaa mimi siyo shuzi lake. Maana hanilipi kwa kumjibu kwenye utopolo wake
Sio lazima ujibu,unaweza soma ukapita kimya kimya
 
Sio lazima ujibu,unaweza soma ukapita kimya kimya
Mwanaume kulalamika lalamika ni dalili ya udhaifu.

Halafu usijitie ukiranja wa kunipangia la kufanya. Wewe unga mkono kivyako. Mimi napinga kivyangu.

Mnawalalamikia wanawake huku mkiendekeza taamaa zenu za kizinifu.

Piga nyeto hautoingia gharama ya kulipia chakula kisha kisiliwe
 
Hapa nazani Kuna tatizo ndio sehemu ya kuangalia Kwa Makini

Nakumbuka tukiwa wadogo nyumbani Tulikuwa tuna dada wa kazi alikuwa na Tabia hio

Bi mkubwa alikuwa ananunua Kg 50 za mchele Sukari kg50 Maharage yalikwepo ya kutosha Mahindi yapo ya kutosha

Lakini hata miezi miwili haifiki Mchele na Sukari na mafuta unakuta yameisha kuja Kufanya uchunguzi Kumbe huyo Dada alikuwa anapika chakula kingi alafu anwaga anagawa vitu Kwa marafiki zake kuanzia mchele Hadi Maharage I mean Kila kitu

@memmata alingalie hili Kwa umakini

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Hahahah sisi tuna ndugu wakifika nyumbani wanakwambia wao hawali kande au Maharage wakati maisha yao huko Wanakotoka ni Kwa Hovyo kweli

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Aah kumwaga chakula siyo vizuri, inabidi mtu ujue kukadiria bana na hata kikibaki basi kitunzwe vizuri kwa matumizi ya baadaye. Chakula kakimwagwi ni dhambi hiyo watu wanatamani hata wapate uji tu wewe unatupa chakula😒

Hapo kwenye kutolewa out then unakula kidogo unaacha, mimi nikishiba naomba kufungiwa kitanisaidia nikirudi home, kwanza tuchakula twa out hata siyo twingi hivoo, nakula namaliza vizuri tu, kuku nusu anishinde? Aah wadada tuache kuigiza maisha 😂 ukirudi home unafakamia kiporo kikubwa eti kuku wa out unashindwa kumaliza.
 
Wewe huna tamaa,akilalamika wewe inakuuma nini?
 
Hii ni changamoto hasa kwa familia ambayo bado inajipanga kimaisha, Unakuta asilimia kubwa ya kipato inaishia kwenye mahitaji ya nyumbani.

Mama wa watoto wangu huwa namwambia kwa uharibifu huu isingekuwa watoto kuna wakati nigegoma kutoa matumizi kabisa.
 
Basi atumie chakula vizuri la sivyo atapimiwa
Kuto tumia chakula vizuri ni kawaida kwa wanawake waki Afrika, Mama yangu mimi anayo tabia hiyo utakuta ana pika ugali mwingi tunakula mwingine ana utupa asubuhi alijitahidi kupika chakula kidogo alishindwa mpa leo akipika chakula lazima kibaki na asubuhi kina mwagwa, Mara nyingi ni ugali maana wali ukilala ni rahisi kuliwa tena asubuhi kuliko ugali.
 
🥲I feel you ..Saivi ndo nakumbuka enzi tukiwa wadogo mama akiwaekea chakula mkashindwa kumaliza mnapanga mstari mnafungua mdomo mnalishwa kilazima 😅nilikua nachukia ila nimekua sasa namuelewa na naishi na hio mentality.
 
Kama kusema nilishasema sana sasa hivi naumia tu maana ukizidi kuongea hawachelewi, utasikia "We mwanaume una gubu kweli, mambo ya jikoni yana kuhusu nini
Inasikitisha sana mwanaume kukosa sauti kwa familia yako..
 
Mpinge ila usimshangae akilalamika kana kwamba ni jambo jipya duniani
Bado ndugu yangu una taabu

Huwezi kunipangia la kufanya na la kuongea.

Ishi kwenye mstari wako and am doing my way
 
mtu asiyejua bajeti ni wa kumwogopa,dawa yao ni moja hakuna kumwaga chakula,yaani hiyo ni order nikikuta mnamwaga chakula nawakatia huduma imeisha hiyo,.ama wazoeshe kutumia vipimo kulingana na idadi yao.
Bora hata wewe kuna huyu ndugu yangu yeye ndani kuna kuku,badae anahamu ya kitimoto,mshahara 500 per month
 
Tunapoishi ni mbali kabisa na familia zetu labda kama anagawa kwa mashoga zake na kwa majirani zangu sina shaka nao sababu ya life style zao. Lakini nisitoe majibu mapema nitalifanyia kazi pia
Kuna rafiki yangu mke wake huwa anawauzia majirani mchele, mkaa, mafuta nk. Jamaa huwa analalamika vitu vinaisha mapema lkn nashindwa kumwambia kwamba mke wake huwa anauza
 
Kuna rafiki yangu mke wake huwa anawauzia majirani mchele, mkaa, mafuta nk. Jamaa huwa analalamika vitu vinaisha mapema lkn nashindwa kumwambia kwamba mke wake huwa anauza
Wewe sio jirani mwema hata kidogo!

Tena unasikia mwanaume mwenzako analalamika hlf unakausha
 
Kulalamikia vitu kama hivi ni ushamba
kwa mtu mwenye malengo ya mbele,kwa mtu asiye na malengo anaishi ilimradi tu ndo atasema ni ushamba,na pia nikupe siri tu hata matajiri unaowaona leo wanamwaga bia ni watu wa bajeti sana,yeye hata mia anataka ajue imetumikaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…