Kwanini wanawake sio wateja wa kahawa inayotembezwa na wagogo?

Mbochong'a

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2011
Posts
767
Reaction score
1,312
Salaam wakuu, kama kuna mtu ana sababu za kitabibu au kisaikolojia naomba atujuze.

Mnisamehe kama hii mada sio ya hili jukwaa na kama ilishawahi kujadiliwa.
 
Kuna mmoja hapa maskani anakuja na jagi kabisa! Na lazima aonje kama ina vigezo
 
Ni wapenz wa kahawa mbona.

Sema wao huwa hawanywei kwenye vijiwe, wananywea nyumbani,

Zile kahawa za product za wazungu.
 
Bibi yangu huwa anajitengezea mwenyewe kahawa, aliyo lima.

Yupo vizur kiafya, hasumbuliw na magonjwa ya uzeeni kabisa
Salaam wakuu, kama kuna mtu ana sababu za kitabibu au kisaikolojia naomba atujuze.

Mnisamehe kama hii mada sio ya hili jukwaa na kama ilishawahi kujadiliwa.
 
Bibia yangu huwa anajitengezea mwenyewe kahawa, aliyo lima.

Yupo vizur kiafya, hasumbuliw na magonjwa ya uzeeni kabisa
Oookey, nimekusoma mkuu, yeah ni kweli sababu hawakai vijiweni ndio maana hatuwaoni!
 
Kumbe watembeza kahawa ni wagogo..
 
Hivi ni wagogo tu ndio watembeza hii kitu ee!!!?
 
Tangu lini Kahawa inakuwa nyeusi.....? Ukiuliza wanakuona wewe Mshamba.. Ninachokiona watu wengi wanalishwa Mkaa wa Kahawa wanakaanga Kahawa mpaka ladha inaondoka.....Kwa maana hiyo kwa ujinga wa kuogopa kuonekana Mshamba wamakunywa Sumu iliyopo kwenye Mkaa....
Hivi ni kweli Ladha ya kahawa ndiyo ile kweli.......?
 
Swali zuri sana, ngoja aje anaefahamu huu weusi na uchungu wa kahawa unatoka wapi na una madhara gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…