Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Tuhuma za uhaini zinahitaji tafsiri sahihi ya msamiati wa "uhaini" kabla haujatumika kuadhibu wale ambao Chadema au kikundi chochote kile ambacho kinatofautiana na watuhumiwa husika. Uhaini ni kufanya mipango ya siri ya kuleta mageuzi ambayo yanapingana na utaratibu uliopo wa kuleta mageuzi ndani ya taasisi au nchi yoyote ile.
Tukiangalia waraka wa Dr. Kitilya akiwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema waraka wake aliutoa ndani ya Kamati Kuu ya Chadema ili ujadiliwe hivyo haukuwa siri na hauwezi ukaitwa ni uhaini. Pili Kamati Kuu ya Chadema ilikuwa na uwezo wa kuukubali au kuukataa bila ya kuathiri masilahi ya mjumbe wa Kamati Kuu ambaye alikuwa amewapa changamoto.
NIONAVYO MIMI:-
BAADHI YA KHOJA ZA MSINGI AMBAZO CHADEMA NI LAZIMA IZITOLEE MAJAWABU ni hizi zifuatazo:-
1) Marekebisho ya Katiba ya Chadema kwenye nyanja hizi hayakwepeki.
a) Kura za maoni za wanachama zitumike kuteua viongozi wa ngazi zote wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama au serikalini badala ya kutegemea vikao vya wachache ambavyo siyo shirikishi na demokrasia yake ni kiduchu kabisa.
b) Viongozi wataondolewa madarakani kwa vikao vilivyowateua badala ya Kamati Kuu ambayo siyo chombo cha uteuzi. Kamati Kuu hujivika gamba la kuwanyang'anya nyadhifa viongozi wasiowapenda wakati wao hawakushiriki katika kuwachagua na kwa kufanya hivyo misingi ya kidemokrasia inakuwa imekiukwa kabisa.
c) Watendaji ndani ya chama wawe ni wataalamu wakiajiriwa kushika nafasi hizo kwa vipindi visivyozidi miaka mitano.
d) Wanasiasa wasishikilie nafasi za kiutendaji ili kutofautisha nafasi za kisiasa na kiutendaji kwa malengo ya kuboresha tija ya uwajibikaji.
e) Asiwepo kiongozi mwenye kofia mbili ndani ya chama ili kutoa mwanya wa kupanua wigo la ushiriki wa wanachama wengi zaidi katika nafasi ya kukiongoza chama chao.
f) Taarifa za mapato na matumizi ya chama zijadiliwe, kuhakikiwa na kupitishwa pia na vikao vya chama kuanzia kata badala ya sasa kuwa ni hodhi ya wakubwa wachache katika kamati Kuu ya chama.
2) Kuvumiliana ndiyo ukomavu wa kisiasa.
Maoni waliotoa akina Dr. Kitilya ni changamoto ambazo zilipaswa zipelekwe ndani ya vikao vyote vya chama kuanzia kata ili vijadiliwe na maoni yapatikane ya kuboresha utendaji wa chama badala ya Kamati Kuu kukimbilia kwenye vyombo vya khabari na kuutusi kuwa waraka ule ulikuwa ni uhaini!
3) Hakuna ambaye ni mkamilifu.
Inashangaza sana kuona wale ambao wanatuhumiwa kwa wizi na ubadhirifu wa mali za chama ikiwemo kujilimbikizia mali wanakua mstari wa mbele kuwanyoshea kidole wale ambao wanawakosoa kuwa ni wezi wa mali ya umma!
4) Misingi ya haki na ya kidemokrasia ndiyo itawaimarisha siyo kuwadhoofisha
Ipo dhana potofu ndani ya Chadema kuwa kupanua wigo la demokrasia kutakaribisha mahasimu wao wa CCM kuitumia kuwavurugia na hivyo kuwadhoofisha na hivyo kujenga utaratibu wa vikao vya juu kuwa na hadhi ya "wenye chama"!
Khali hii kamwe haitakiimarisha Chama bali kukidhoofisha kwa sababu wanachama wa kawaida huwezi tu kwenye majukwaa ukawasifia kuwa nguvu iko kwao yaani "PEOPLE'S POWER" wakati huwashirikishi kwenye maamuzi ya kukiendesha chama chao hususani ya kuteua, kudhibiti na kuwaasa viongozi wao ambao waliwachagua wao wenyewe.