Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Mabibo Beverages Distributors wamekuwa wakitishia umma kuwa wanaotaka kufanya biashara ya kinywaji cha WINDHOEK ni lazima wawe mawakala wao kwa madai wao wana mkataba na wamiliki wa kinywaji hicho kuhodhi hiyo biashara hapa nchini.
Mwaka 2009 walikimbilia mahakamani ambako walitangazwa kuhodhi biashara hiyo na uamuzi huo wao wanaona ndiyo umemaliza ubishi juu ya suala hilo na sasa wanaitishia FCC- FAIR COMPETITION COMMISSION kuwa wataiburuza mahakamani kama hawatafuta tangazo lao kwenye vyombo vya khabari la kuwataka wale wote ambao wanataka kusambaza kilevi hicho kupitia kwa FFC badala ya Mabibo.
TATIZO LIKO WAPI?
1) Uamuzi wa kimahakama haukuwahusisha FCC na hivyo ni makosa kwa Mabibo kudai FCC wanawajibika kuheshimu amri ya mahakama. Kama Mabibo wangelitaka uamuzi huo uwabane FCC walipaswa kuhakikisha wamewajumuisha kwenye kesi hiyo kabla ya kusikilizwa.
2) Uamuzi ambao mabibo wanatudobosha nao ni uamuzi wa mahakama ya hakimu mkaazi na wala siyo wa mahakama ya kileleni na kwa vile unagusa watu wengi ambao hawakuhusishwa moja kwa moja na uamuzi ule basi siyo sahihi kuutumuia uamuzi tajwa kama ngao ya kuwazuia FCC kutoa vibali kwa wafanyabiashara wengineo ambao wangelipenda kushiriki kwenye biashara hiyo.
3) FCC wanabanwa na sheria inayoiunda taasisi hiyo kuwa ni lazima walinde ushindani wa kibiashara hapa nchini ili kumlinda mlaji. Hata kama kuna mikataba ambayo Mabibo iliingia na WINDHOEK ambayo inatishia haki za mlaji kama kupata huduma tajwa kwa bei ya soko basi ni jukumu la kisheria la FCC kuhakikisha mikataba hiyo inatamkwa inakinzana na sheria zetu ambazo lengo lake ni kuhakikisha ushindani hauathiriwi na mikataba feki kama hiyo.
4) FCC inapaswa iendelee na kutoa vibali kwa makampuni ambayo yangelipenda kufanya biashara tajwa au vinginevyo atakuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao.
5) Kama Mabibo wanaona hawaridhiki basi waache vitisho na kutinga mahakamani na kuwashitaki FCC badala ya kutoa vitisho ambavyo vinaashiria wanajua wanachofanya siyo haki mbele ya sheria.....................