Kwanini wasanii wa kike hawaolewi na hata wakiolewa hawadumu ndani ya ndoa?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Wakuu,

Kuna hawa wasanii wa kike wamekua wakiishi bila ya kuolewa na ikitokea wameolewa basi hawafikishi miezi 6 wanaachwa. mifano ipo kibao hapa bongo kuna huyu Komandoo lady na wengineo ya sijui wana gundu.

Kuna baadhi wamefikia hatua wanajivalisha pete wenyewe hili kutoa gundu cha ajabu hawa wadada ni warembo hatari mfano; Aunt,Uwoya.Wema.lakini sijui labda hawajawapata type yao.

Tujuzane hapa
 
Sikujua kama Jide hakufikisha miezi 6 kwenye ndoa
 
mkuu ya kwangu ina miaka 9 sasa.na bado inapeta

The best thing is, are you happy? Kama una furaha na si maigizo au kumuogopa "padiri" na kile kiapo then fine. Nilimpoteza dada yangu miaka 3 iliyopita kwa kuvumilia mateso katika ndoa yaliyosababisha kiharusi. Tulimshauri sana aondoke kwa mumewe kwa mateso aliyopata hakutusikia.

Mara ya mwisho alipigwa sana. Aliacha watoto 4 ambao mwelekeo wa maisha yao umeharibika kabisa kutokana na mama kuwa mhimili mkuu wa familia ile (alikuwa mwalimu). Kwa kweli baada ya kifo cha dada yangu siwezi kumlaumu mwanamke au mwanamume yeyote anayetengua kiapo cha ndoa hata kama amekaa mwezi mmoja tu. Mtu anavumilia utadhani ndoa imefungwa na
Malaika Gabriel... Kha!
 
Oh basi hongera wewe na mumeo.
Huyu NN ni mtata kama nini .... yeye hoja zake ni ngumi mkononi , ustaarabu kwake ni nadra sana ....hiyo hongera kaitoa kwa kejeli kwa nina uhakika hajui kama wewe( lukelo sakafu ) ni mwanaume ama mwanamke. Hivyo hakutakiwa kutumia neno mumeo hapo.
 
Last edited by a moderator:
Huyu NN ni mtata kama nini .... yeye hoja zake ni ngumi mkononi , ustaarabu kwake ni nadra sana ....hiyo hongera kaitoa kwa kejeli kwa nina uhakika hajui kama wewe( lukelo sakafu ) ni mwanaume ama mwanamke. Hivyo hakutakiwa kutumia neno mumeo hapo.

Mpongeze mwenzio kwa kuitunza ndoa na mume.
 
Mpongeze mwenzio kwa kuitunza ndoa na mume.
Unajua wakati mwingine uzoefu wa maisha usipokuwa makini waweza kukufnya uonekane kuwa punguani hasa hasa maeneo ya watu waliostaarabika.

Katika JF ukikuta ID ni ya zamani mfano 2006 unatarajia kupata maoni yenye busara, maana inasemwa kuwa waliokuwepo wakati wa Jambo forum walikuwa wanashusha pweiti za kutosha za kuwa zindua watanzania kutoka fikra mgando kwa staha ya hali ya juu. Lakini inashangaza sana NN mbali na uzoefu wote huu wa kushiriki hapa JF (posts 49 961) bado anaendelea kubadilika kifikra kutoka mbaya kwenda mbaya sana hasa linapokuja suala la utumiaji wa lugha ya kiuungwana.

Ndiyo maana nasema uzoefu wa maisha ya maeneo fulani unaweza kukufanya uonekane punguani maeneo mengine. Eneo analoishi NN linaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye kuharibu uwasilishaji wa kistaarabu wa hoja zake hapa JF.
 

We nawe hebu kwenda zako huko na haya mahubiri yako.....
 
We nawe hebu kwenda zako huko na haya mahubiri yako.....

Nimefurahi sana kwani ujumbe umekufikia sawia kiasi cha kuhangaika na JF rep.

Ebu ufanyie kazi basi huo ujumbe....anza kuleta hoja zako hapa JF kwa lugha ya kistaarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…