Kwanini wasanii/wanamichezo wetu wanaogopa kwenda na familia zao kwenye matukio muhimu?

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
416
Wakuu tusaidiane hapa,

Ni kwanini wasanii wetu hapa Bongo wanaogopa kuongozana na familia zao katika matukio muhimu mfano wanapoenda kuchukua tuzo za aina mbalimbali wanaenda peke yao tu tofauti na wasanii wa marekani kama kina P.didy, Snoopy dog doy,jamie fox, ambao upenda kwenda na watoto wao kuchukua tuzo zao.

Hata kwa upande wa wanasoka wetu hawana kasumba ya kuongozana na watoto au wake zao kwenda kuchukua makombe au tuzo zao tofauti na kina, Drogba, John terry, Frank Ribery, Ronaldo, Messi, Steven Gerald ambao huongozana na familia zao kwenda kuchukua tuzo zao.

Je, wabongo wanaogopa nini hapa?

Wanaojua kwa kina karibuni tujuzane hapa...
 
Ni maamuzi tu, waige kila kitu cha wazungu??
Mwishowe wataiga ushoga pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…