Elections 2010 Kwanini wasimamizi wanatukunjia karatasi za kura?

Elections 2010 Kwanini wasimamizi wanatukunjia karatasi za kura?

Msongoru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2008
Posts
306
Reaction score
24
Moyo wangu umeshtushwa ghafla baada ya kuulizwa swali hili! hvi kuna madhara yoyote kama wale wakikukunjia?

Na ni kwanini wanatoa karatasi zikiwa zimekunjwa? Je kuna uwezekano wowote wa kura yako kuhamishwa?
 
Ili mkunjo uwe wa aina moja kwamba sio kila mtu akunje anavojua nathani itakuwa ivyo lakini haina athari yeyote ile.
 
Haina Madhara mmkuu tuliza moyo ushindi ushaonekana toka asubuhi
 
Nimeshapiga nimechunguza yale yaliyosemwa hapa JF kuhusu karatasi . Nimeona sivyo hamna cha gundi wala nini. ushindi tu
 
Mie pia imenipa wasiwasi sana, kuna mwana JF mmoja aliwahi kudokeza tetesi za kura kuhamia upande mwingine. sina uhakika ila tusubiri maana tukiona tofauti imekuwa kubwa tutajua hizo ni trick za technology ya hali ya juu. Nilikaa km dk 5 katika chumba nikijaribu kusoma mazingira na athari inayoweza kuletwa na mikunjo hiyo.kabla ya kupiga, niliikunja kuona mwelekeo wake, sikugundua kitu. Kama kweli upo uwezekano huo basi hii ni sayansi ya hali ya juu. nilishawahi kusikia huko Amerika ya kusini ilishawahi tokea hali kama hii ya kura au tick kuhamia kwa mgombea mwingine.Ila proofs sijawahi kuziona labda wataalamu zaidi watatusaidia. kwa vyovyote vile hali itajulikana tu nadhani tusiwe na wasiwasi juu ya hilo.
 
kama vipi baada ya kupiga kunja tofauti na alivyokunja yeye. Mi nimefanya hivo...
 
Ili mkunjo uwe wa aina moja kwamba sio kila mtu akunje anavojua nathani itakuwa ivyo lakini haina athari yeyote ile.

Kwani wapiga kura hawakuambiwa jinsi ya kukunja karatasi? Chama Cha Majambazi waendelee tu na sarakasi zao lakini siku ya kufa miti yote huteleza na hii dhuluma itakuja kulipwa hapa hapa duniani.
 
Mimi pia nimetumiwa msg inayosema inatoka sehemu nyeti kuwa tick inahama kwa technology na kuwa bora kukandamiza kwa sehemu ya kuweka tick ili kuondoa hizo chemicals ambazo zinananata kidogo ukikandamiza. Naamini ufuatiliaji utafanywa ili asije mtu akawa na ajenda yake na kutuchagulia bomu. kama kufuatilia ni sasa wakati kura zinapigwa. Kwa mfano wale walio vituoni wanaweza kupiga sampla vote na kuicha nje bila kuitumbukiza kwa muda ili kuona kama inabadilika au la. Kama kuna possibility ya kura kuharibika basi hiyo iharibiwe makusudi ili kufuatilia kama labada baada ya masaa kadhaa kuna reaction yoyote inayotokea kufuta yale yaliyoandikwa awali na kutokea alama mpya. Ni bora tuwe scientific. si vizuri kunyamazi tetesi.
 
nahisi kama uwezekano ni mdogo, labda kuharibu kura maana ikihama lazima na kwako ibaki.
 
........mimi nilibadilisha ule mkunjo maana nachojua mimi karatasi inakunjwa ili kurahisisha kupenya kwenye tundu la box so nitakunjaje hiyo ni suala langu so nilikunja kwa namna tofauti as long as ile mihuri yao ilikuwa juu.
 
Nilibadilisha mkunjo wa karatasi ya nafasi ya udiwani. Nadhani hamna shida sana
 
Moyo wangu umeshtushwa ghafla baada ya kuulizwa swali hili! hvi kuna madhara yoyote kama wale wakikukunjia?

Na ni kwanini wanatoa karatasi zikiwa zimekunjwa? Je kuna uwezekano wowote wa kura yako kuhamishwa?

Mimi nilishtuka pia. Lakini nikasema kimoyomoyo: Nitaifunua. Nitapiga. Nitaikunja. Nitaikunjua. Nitahakiki. Then nitakunja tena.

I did so na sikuona tatizo
 
hakuna tatizo lolote, ushindi wadau uko wazi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Ni uvumi mimi nilihakiki kwa kuscaratch two times kwenye kibox cha Slaa ili kama kuna gundi itoke sikuona kitu.
Kukunja karatasi nilifanya mwenyewe
 
tatizo ni wasimamizi ni wachovu,nina wasiwasi na uzalendo wao,hasa kama mshiko wa kati ya laki2-8 utapitishwa.
nimescratch kuhakiki naona hamna kitu,labda karatasi ijifute tiki ktk sehemu ya chadema and tiki ijitokeze ktk sehemu ya CCM,kwani kalamu wanakupa wao,so u never know the trick could be with the pen ink
 
Back
Top Bottom