Sababu zipo nyingi.
1.Magazeti mengi ya siasa kuripoti bila kufanya uchambuzi/kuingia kwa undani,bado yanaripoti kama vile tuko miaka ya mwanzoni mwa 2000 ambako hakukuwa na Facebook wala Instagram mf.gazeti linaandika mtu asiyejulikana ameua Polisi 3 bila maelezo ya ziada wao wanategemea vyanzo kutoka vyombo rasmi na hivyo vyombo rasmi vinaweza kutokutoa maelezo ya kina ya tukio au wakatoa kwa uchache,wakati mtandaoni wameandika jina la huyo mtu,anapoishi,kazi yake,sababu za kuua,picha mbali mbali za huyo mtu,wanaweka hadi video nk. Na hiyo habari unaipata muda huo huo wakati tukio linafanyika,habari kama hiyo gazeti linatoa kesho yake.Jiulize nani atanunua gazeti la namna hiyo.Tofauti na habari za michezo magazeti ya michezo yanafanya uchambuzi mfano juzi Yanga ilivyofungwa na Kelvin Kapumbu magazeti ya michezo hayakuandika habari za Kapumbu kuifunga Yanga bali yalichambua na kuandika kwa kina tamasha lilivyokuwa na jinsi mchezo ulivyochezwa habari ambazo huzipati mtandaoni.
2.Magazeti mengi ya Siasa yanaandika habari za kujipendekeza Serikalini, na hili lilianza wakati wa awamu ya tano.Hiyo pia ni sababu ya kukosa wasomaji.
3.Magazeti ya siasa kubanwa sana na sheria,kanuni nk.Na kwa sababu yenyewe yanaandika habari zinazoweza kuleta athari kwa wanasiasa/watawala na ni rahisi kuyadhibiti kwahiyo yanalazimika kuandika habari nyepesi nyepesi ambazo hazina mvuto tofauti na magazeti ya michezo ambayo habari zao hazina athari kwa watawala.
4.Wananchi kukata tamaa na habari za siasa/watawala,wanaona mambo ni yaleyale wanaongopewa kila siku mara uchumi umekua wakati wao mifukoni hakuna kitu.Wanaamua kusoma habari za michezo au kujihusisha zaidi na michezo ambako kunawapa faraja kwa kiasi fulani.