Kwanini wasomi tuaongezeka lakini Taifa bado ni maskini ?

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Ni dhahiri kabisa hapa Tz kuna ongezeko kubwa sana la taasisi za elimu za taaluma mbalimbali sambamba na ongezeko la wahitimu, Je, tunakosea wapi? Hatuzijui fursa? Ni kweli taasisi za mikopo zina masharti magumu sana?au mawazo ni kuajiriwa tuu?

Tukumbuke tu juzi hapa wenzetu wa Uganda wametengeneza gari wenyewe,Wakenya wanatuuzia madawa mengi tu waliotengeneza wao, Nchi kama S.Africa leo wana workshorps za kutengeneza magari na vyombo wakadha vya moto.Watazame nchi ya Irani leo wanalalamikiwa na dunia nzima kwa kutengeneza silaha za nuclear kwa kutumia wataalam wao, Je, inawezekana waalimu wetu hawatuandai vizuri?

Mtu unajiita engineer au doctor, ama mchumi huna chochote ulichobuni mpaka unazeeka zaidi unategemea kamshahara ka serikalini. Hebu vijana tushauriane tutatokaje hapa?
 
Asante sana ndgu yangu kwa kuwakilisha maoni yangu kama inavyotakiwa, yaani umekuwa kama umo kwenye fikira zangu.

asante kwa good topic!

subiri
narudi sasa hivi na sababu kibao!
 
Ubishooo mwingi watu wanajua ukisoma wewe ni bosss hawajui ukipata elimu unapaswa kuutumia huo ujuzi ufsnye kazi
 
Asante sana ndgu yangu kwa kuwakilisha maoni yangu kama inavyotakiwa, yaani umekuwa kama umo kwenye fikira zangu.

asante kwa good topic!

subiri
narudi sasa hivi na sababu kibao!

Twapaswa tushauriane tutatokaje hapa ndugu! Je,ni nani wa kutandikwa mjaledi mambo yaende?
 
Hata mimi nilikuwa napata shida sana nini maana ya elimu,siku moja nilimsikiliza marehemu Dr. Myles Munroe anasema kupata elimu inafanana na mtu anayeng'arisha viatu,ni lazima uwe mwerevu kwa kuzaliwa ili utakapoongeza elimu iweze kuwa na manufaa kwako.

Kwa hapa Tanzania inaonyesha wazi kuwa mfumo wa elimu yetu umeshindwa kuendeleza vipaji ambavyo tayari wanafunzi wanavyo.
 

Ni kweli mkuu umenena sana!
 
Elimu yetu haitujengi kuwa na hali ya uthubutu. Tuko kinadharia sana na pia tunapenda kuwa on the safe side. Kutokana na elimu yetu na jamii ilivyo na mtazamo finyu, sehemu kubwa ya jamii inaamini msomi unatakiwa ukakae ofisini na sio kuchafuka mikono.

Ingependeza somo la ujasiriamali liwe la lazima kuanzia shule za msingi mpaka vyuoni. Kwa kufanya hivi, angalau wachache watafumbuliwa macho.
 
Kuna haja ya kutumia kingereza katika elim yetu? kama ipo je inafaida gan wakati wakati mwingi maofisini tunatumia kiswahili?
 

Enzi za RTC nilikuwa mdogo, mzee mmoja kijijini kwetu nilimsikia akisema "Nataka mwanangu akienda shuleni Tosamaganga akasomee masomo ya RTC", enzi hizo RTC ilikuwa ujiko sana. Sikujua ana maana gani.

Ukija ktk hali halisi,wengi wetu tuliambiwa tusome ili tuje tuwe akina fulani serikalini basiiiiiii. Hilo pia ni moja ya matatizo makubwa sana. Wakati namalizia masomo shule fulani,rafiki yangu mmoja alisema, " mimi naenda kufuga kama baba anavyofuga", mimi nikasema nabaki Dar, mkoani sirudi. Tofauti ya maisha kt yetu ni kubwa sana, mimi nawaza kodi ya nyumba, mwenzangu anatafuta kiwanja K/koo.

Namna ya kufikiri kwetu,kutenda kwetu,malengo yetu,malezi yetu, matumizi ya rasilimali zetu ni changamoto kubwa, serikali inafuata baada ya wewe mwenyewe kujiweka sawa.
 
Nchi yetu kwa ujumla bado hatujawekeza kwenye elimu ipasavyo.

Tume base kwenye theory zaidi, mfano, kitabu cha form 3 physics (usaid) topic ya light kimeeleza jinsi ya kutengeneza, microscope na telescope, lakini jiulize, wangapi wametengeneza?

Syllabusi inahitaji tutengeneze telescope, lakini fungu lililo wekwa haliruhusu kufanya hivyo.

Pia elimu yetu ni elimu ambayo duh......cjui niieleze vp, maana unakuta hata practical za osmosis watu wanashindwa kuzifanya.

Kiufupi, elimu yetu, ime base kwenye theoretical issues than practical issues, ndio maana watanzania, kwenye sekta ya kutoa sababu tuko juu sana na tunauwezo wa kuelezea habari kama tulikuwepo kwenye tukio halisi.

Hatuna moyo wa kujisomea, na tukitaka kusoma basi tutaishia kusoma udaku tu, ukitaka kuthibitisha nenda kwenye sehemu ya magazeti na uangalie watu wengi wanasoma vichwa vipi vya habari.

Asomacho mtu, ndicho kimjazacho kichwani mwake (akili yake).

Swali jingine, katika taasisi tofauti za elimu, hasa zile zinazo husisha practicals (zile zenye maabara), i.e shule zetu za sekondari, je walimu wangapi wana maabara zao kwaajili ya kufanya uchunguzi zaidi?. Na hizo maabara zina vifaa vya kutosha?

Tulikuwa na shule za agriculture, ufundi na za biashara ila kinacho endelea kinajulikana.

Mambo mengi yanazingua, mwisho wa siku tunasema, elimu yetu inatuandaa kufanya kazi za maofisini za kushika makaratasi pekee na sio practicals.
 
Kuna jamaa aliwahi kusema sisi watanzania ni wavivu wa kusoma! Hii kauli iliniuma sana na ilikua changamoto kubwa sana kwangu.
 
Elimu siyo vyeti, ni kile unachobaki nacho baada ya kuhitimu masomo yako, na kiweze kukusaidia kupambambana na mazingira uliyo nayo.
 
Kwanza tungeanza kuulizana swali la kwanza "msomi" ni nani (at least ktk Tanzanian context)?
 
Kuna jamaa aliwahi kusema sisi watanzania ni wavivu wa kusoma! Hii kauli iliniuma sana na ilikua changamoto kubwa sana kwangu.

Ni ukweli, na inabidi uwe na roho ngumu kuukubali.

Watanzinia sio wavivu tu kusoma, bali pia, tupo wavivu sana kufanya kazi, hatujitumi ipasavyo.
 
Mfumo wetu wa elimu ndo mbovu,mfano watu wengi wanasoma dgree sio zao kwasababu tu ya kupata mkopo so automatically unaua vipaji vingi vya watu ambao walikuwa na uwezo kwenye sekta flan lkn kwasabab kozi anayotaka kusomea cyo kipaumbele cha serikal inambidi tu abadil mwelekeo,vilevile dunia inabadilika kila siku lkn mfumo wetu wa elimu haubadiliki kulingana na mahitaji ya dunia ya sasa,hivyo basi huko mashuleni na mavyuoni tunafundishwa vitu ambavyo hauwezi kuviapply kwenye maisha yetu halisi!
 
Tuko nyuma kwa kuwa elimu yetu ni elimu ya ukimbizi kama alivyoiita Mwalimu Juliasi Nyerere, watu wanasoma ili wawe watu fulani katika jamii na sio waje kutoa suluhisho la matatizo ya jamii.

Walikokimbilia wadau kwenye sayansi na uundaji wa mashine ni mbali sana, yapo matatizo ya kawaida kabisa ambayo wasomi wakimbilia mijini wameyashindwa. Waliopita shule wanaamini wao ni bora kuliko ambao hawakupita shule na wasiopita shule wanawaaminia waliopita ambao kimsingi ni waganga njaa kama wao ila kwa namna tofauti.

Tukiubadili huu mtazamo huhusu wasomi/wasiosoma tunaweza kupiga hatua kidogo...
 
huyu marehemu nilikuwa namkubali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…